Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Hawaii yafanyia jaribio king'ora cha kuonya shambulizi la nyuklia

MTEULE THE BEST Hawaii yafanyia jaribio king'ora cha kuonya kuhusu shambulizi la nyuklia Kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita baridi jimbo la Hawaii nchini Marekani limefanyia jaribio king'ora cha kuonya kuhusu shambulizi la nyuklia Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa na Korea Kaskazini mapema wiki hii. Hawai kawaida ina ving'ora ambavyo huonya kuhusu majanga ya asili kama tsunami. Kingora cha nyuklia kina mlio tofauti ambacho huwaonya watu kusalia manyumbani wakisubiri ushauri zaidi. Lakini king'ora hicho kilisikika tena Ijumaa na kitarudiwa klila jumatatu ya kwanza ya mwezi. Kombora linalorushwa kutoka Korea Kaskazini linaweza kushambulia Hawaii ndani ya dakika 20 baada ya kufyatuliwa. Hivi majuzi Korea ilifyatua kombora mpya la masafa marefu ambalo inadai kuwa linaweza kushambulia ndani ya Marekani. Kombora linalorushwa kutoka Korea Kaskazini linaweza kushambulia Hawaii ndani ya dakika 20 ...

Rais wa TFF ateuliwa ndani ya CECAFA

MTEULE THE BEST Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika Baraza la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Desemba 2, 2017 jijini Nairobi, Kenya Rais Karia alipita bila kupingwa baada ya wanachama watatu kati ya nane kujitoa hivyo watano waliobaki kuchaguliwa bila kupingwa. Wajumbe hao ambao wataungana na Rais wa CECAFA, Mhandisi Mutasim Gafar wa Sudan watakuwa na kibarua cha kuboresha utendaji kazi wa baraza hilo kwa ajili ya kuimarisha soka la Afrika Mashariki na kati. Wengine waliochaguliwa ni Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia) na Mwanamke Petra Dorris wa Kenya.

Nasari avamiwa anusurika kupigwa risasi usiku

MTEULE THE BEST Mbunge wa Jimbo la arumeru Mashariki Joshua Nassari, amevamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha, na kunusurika kupigwa na risasi ambazo zimeua mbwa wake. Kwenye ukurasa wake wa twitter Joshua Nassari ameandika ujumbe akitoa taarifa kuwa watu hao walivamia nyumbani kwake usiku wakiwa na silaha za moto ambazo waliwafyatulia mbwa wake, na yeye kunusurika baada ya kukimbia akiwa na mkewe, kitendo ambacho amesema kimemfanya akose imani na nchi yake. "Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya Usa River usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu", ameandika Joshua Nassari. Kufuatia tukio hilo East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha kupata taarifa zaidi juu ya tukio hilo, na simu yake kuita bila m...

MPIRA ULIVYOBADILISHA MAISHA YA MASTAA 10 HIZI NDO NYUMBA WALIZO KUWA WANAISHI NA ZA SASA 10 Footballers Houses - Then and Now - Ronaldo, Neymar, Messi and

MTEULE THE BESTBEST 10 Goals the Football World will Never Forget_HDHD Magoli bora zaidi duniani angalie hapa MPIRA ULIVYOBADILISHA MAISHA YA MASTAA 10 HIZI NDO NYUMBA WALIZO KUWA WANAISHI NA ZA SASA  Rooney, benzema, messi, Neymar, Ronald  na wengine  angali a mijengo yao ANGALIA HAPA

Mwana michezo unaikumbuka haya TOP 10 GOALS- 2014 FIFA World Cup Brazil™ [OFFICIAL]_HIGH TUKUTANE RUSSIA 🇷🇺 2018

MTEULE THE BEST Magoli 10 bora final za world 🌏  cup 2014 angalia hapa chino

Manula aitumia salamu Libya

MTEULE THE BEST Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara “Kilimanjaro Stars” Aishi Salum Manula amesema kutokuwajua vizuri wapinzani wao Timu ya Taifa ya Libya hakutakuwa chanzo cha kutokufanya vizuri katika mchezo wa awali wa michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya. Manula amesema mara nyingi Kocha hutoa mbinu kwa wachezaji wake kutokana na kuijua japo sio kwa undani timu wanayokutana nayo hivyo wanaamini Kocha anaifahamu Libya na mbinu walizofundishwa zitawasaidia kuweza kupambana nao ili kuibuka na ushindi katika mchezo huo na inayofuata. " Timu ya Libya siijui kwa hivyo lakini nadhani kwa vile ambavyo Mwalimu amatufundisha na mbinu ambazo ametupa kuelekea katika mchezo wetu wa kwanza nadhani tutafanikiwa kwani nadhani yeye ameweza kuifuatilia vizuri zaidi na kwaundani na kujua kwamba Libya ipo vipi ili atupatie mbinu gani na tuweze kuushinda mchezo huo , " amesema. Aishi ameongeza kwa kuwataka watanzania kuendelea kuwapa sa...

Wema Sepetu aondoka rasmi Chadema

Muigizaji wa filamu za kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu ametangaza rasmi kurudi Chama Cha Mapinduzi huku akidai kwamba hawezi kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amesema kwamba anatangaza rasmi kuondoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambacho alitangaza kujiunga nacho Februari mwaka huu "Siwezi Kuendelea kuishi kwenye nyumba inayo nikosesha amani... Peace of mind is everything for me. Natangaza rasmi kuondoka Chadema na kurudi nyumbani" . Wema Sepetu.