Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SAMATTA

Droo UEFA na Europa League hii hapa

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England Manchester City wamepangiwa kucheza na klabu ya Schalke ya Ujerumani katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya droo kufanywa. Manchester United wamekabidhiwa miamba wa Ufaransa Paris Saint Germain. Mabingwa hao watetezi wa ubingwa Ufaransa hawajashindwa msimu huu ligini nyumbani ambapo wanaongoza wakiwa na alama 44 kutoka mechi 16. Wana washambuliaji nyota kama vile Neymar, Kylian Mbappe na Edison Cavani. Walimaliza viongozi Kundi C, kundi ambalo lilikuwa na Liverpool, Napoli na Red Star Belgrade katika hatua ya makundi. Lakini walishindwa na Liverpool uwanjani Anfield. United hawajawahi kukutana na Paris St-Germain katika michuano ya Ulaya. Hata hivyo, mashetani hao wekundu hawajawahi kushinda na klabu yoyote kutoka Ufaransa katika michuano ya Ulaya tangu mwaka 2005. Droo kamili: Manchester United v PSG Schalke v Manchester City Atletico Madrid v Juventus Tottenham v Borussia Dortmund Lyon v Barcel...

UMILIKI WA NDEGE WAWANYIMA USINGIZI MASTAA WA BONGO

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva na moja ya kiongozi katika kundi la Tip Top Connection, Madee Alli 'Seneda' ameelezea tamaa yake juu ya kumiliki ndege yake binafsi katika maisha yake. Msanii, Madee (kushoto) na Mwanasoka, Mbwana Samatta (kulia) Madee amesema kuwa ana ndoto ya kumiliki ndege katika maisha yake kiasi cha kumnyima usingizi wake kila siku. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Madee ameandika, " ndoto inayosumbua usingizi wangu ," huku akiwa katika picha inayomuonesha akitembea kuelekea kwenye ndege ndogo. Kauli hiyo ya Madee kuhusu kumiliki ndege inakuja miezi michache baada ya nyota wa soka nchini anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta kueleza matamanio yake juu ya kumiliki ndege yake binafsi. Septemba 12, Samatta katika ukurasa wake wa Instagram aliandika, " ndoto za kumiliki 'Private Jet' zimeanza baada ya kupiga picha hii, sio kila ndoto inaweza kutimia ila acha vita ianze ". Kwakuwa wote ni watu m...

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 30.10.2018

: Mauricio Pochettino, Antonio Conte, Loris Karius, Divock Origi, Jose Mourinho, Ousmane Dembele, Cristiano Ronaldo Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, amesema aliihama Real Madrid na kujiunga na Juventus kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania Florentino Perez hakumfanya ajihisi kama mchezaji anayethaminiwa na kudhaminiwa sana. (L'Equipe, kupitia Express) Real Madrid wanamtaka meneja wa sasa wa Tottenham Mauricio Pochettino awe meneja wao mpya wa kudumu kufikia mwisho wa mwezi huu. Miamba hao wa Uhispania walimfuta kazi Julen Lopetegui baada yake kuhudumu kwa miezi minne na nusu Jumatatu. Alifutwa baada ya Madrid kuchapwa 5-1 na Barcelona Jumapili. (Sun) Mazungumzo ya Real na kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ya kumtaka achukue mikoba ya ukufunzi Madrid yamekwama. Hii ndiyo sababu iliyochangia Santiago Solari ambaye ni mkufunzi wa timu ya akiba kuwekwa kwenye usukani. Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez ni miongoni mwa wanaopigiwa u...

Mbwana Samatta: Sababu ya mshambuliaji wa Tanzania kung’ang’aniwa na klabu za West Ham, Everton na Burnley Englan

Mbwana Samatta: Sababu ya mshambuliaji wa Tanzania kung’ang’aniwa na klabu za West Ham, Everton na Burnley England Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta anang'ang'aniwa na klabu tatu za England, taarifa za vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema. Tetesi zinasema nyota huyo anatafutwa na West Ham United, Everton na Burnley. Samatta, 25, maarufu kwa Watanzania kama Samagoal ameng'aa sana akichezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji. Amefungia klabu hiyo mabao 11 katika mechi 16 ambazo amewachezea msimu huu, nusu ya mabao hayo akiyafunga barani Ulaya. Samatta asaidia klabu yake kufuzu Europa League Utafiti: Mbwana Samatta, Salim Kikeke wana ushawishi mkubwa Tanzania Kylian Mbappe ana uhusiano na Tanzania? Jedwali la Msimamo wa ligi ya EPL 2018/19 Taarifa za kumhusisha Samatta na klabu ya Everton zimetoka kwa mtandao wa hitc.com, mmoja wa mitandao ambayo imeibukia kuwa maarufu kwa taarifa za wachezaji na kuhama kwao. Kwa nini anahusishwa na ...