Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BUNGE

Marekani Itakuwa Chaguo la msingi Iwapo Mkataba wa Madeni Utaanguka - Katibu wa Hazina

Janet Yellen alionya Jumapili kwamba ikiwa Congress itashindwa kufikia makubaliano ya kuongeza kikomo cha kukopa cha dola trilioni 31.4 kufikia wakati huo, italazimika kutolipa "baadhi ya bili" muda mfupi baadaye. "Tathmini yangu ni kwamba uwezekano wa kufikia Juni 15 tukiwa na uwezo wa kulipa bili zetu zote ni mdogo," alisema. "Mawazo yangu ni kwamba ikiwa kikomo cha deni hakitaongezwa, kutakuwa na maamuzi magumu ya kufanya kuhusu bili ambazo hazijalipwa." Siku ya Ijumaa, Rais Joe Biden aliwaambia waandishi wa habari kwamba anafikiria kutumia mamlaka yake ya utendaji chini ya Marekebisho ya 14 ili kupitisha Bunge na kuongeza kiwango cha deni kwa upande mmoja lakini hofu sasa hakuna wakati wa kutosha kufanya hivyo.

Trump Kuchunguzwa na Bunge kwakutumia madaraka vibaya

Spika wa Bunge la Wawakilishi Nancy Pelosi amesema Demokrasia ya Wamarekani iko mashakani, rais anawaacha bila chaguo Spika wa Bunge la Wawakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi anasema bunge hilo litawasilisha mashtaka ya uchunguzi dhidi ya rais Donald Trump, kwa madai ya matumizi mabaya ya mamlaka yake. "Demokrasia yetu iko mashakani, rais anatuacha bila chaguo la kufanya," alisema kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa Democrat. Ameyasema hayo siku moja baada ya kamati ya masuala ya sheria ya bunge kuanza kuangalia mashitaka yanayoweza kuwasilishwa dhidi ya rais huyo kutoka chama cha Republican. Bwana Trump aliwaambia Wademokrats kama watataka kumshitaki basi waharakishe. Alituma ujumbe wa Twitter muda mfupi kabla ya kauli za Bi Pelosi : " Kama mtanichunguza, mfanye sasa hivi, haraka, ili tuwe na kesi ya haki katika Seneti, ili nchi iweze kuendelea na shughuli za kawaida'': Mbunge wa Congres jimbo la California, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari A...

Serikali kujenga mabweni wanafunzi wasipate mimba

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amesema mpango wa Serikali ni kujenga Mabweni katika Shule zote za Msingi na Sekondari, ili kuwanusuru na wanafunzi wa kike na suala la mimba. Mwanafunzi mwenye mimba Naibu Waziri Waitara ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza Bungeni jijini Dodoma leo Novemba 15, 2019 wakati wa kipindi cha maswali na majibu kutoka kwa Wabunge kwenda kwa Mawaziri. Waitara amesema kuwa " mpango wa Serikali ni kujenga Mabweni katika Shule zote za Msingi na Sekondari ili watoto wakike wapate sehemu za kukaa na tuwaepushe na mimba zitakazowafanya washindwe kuendelea na masomo ." Leo Novemba 15, 2019 Bunge hilo linatarajiwa kuahirishwa baada ya kujadili mpango wa maendeleo ya Taifa kwa mwaka ujao wa fedha. Serikali kujenga mabweni ili wanafunzi wasipate mimba.

RAIS APINGANA NA UAMUZI WA BUNGE

Trump akaidi uamuzi wa bunge na kuamua kuiuzuia silaha Saudi Arabia zenye thamani ya $8bn Rais Trump, akiwa pamoja na mwanamfalme wa Saudia wanashika chati inayoonyesha mauzo ya silaha kwa Saudia Rais huyo wa Marekani ametumia kura ya turufu kufutilia mbali uamuzi wa bunge la Congress la kuzuia mauzo ya silaha yenye thamani ya $8bn kwa Saudia na UAE. Donald Trump alisema kuwa maamuzi hayo matatu yatadhoofisha uwezo wa Marekani ulimwenguni na kuharibu uhusiano wake na washirika wake . Hatua hiyo inajiri baada ya mabunge yote mawili kupiga kura ya kuzuia mauzo hayo. Baadhi ya wabunge wanasema kwamba walihofia kwamba silaha hizo huenda zikatumiwa dhidi ya raia katika mgogoro wa Yemen. Wameshutumu vitendo vya Saudia nchini Yemen pamoja na mauaji ya mwaka jana ya mwandishi Jamal Khashoggi. Hatahivyo bunge le seneti litapiga kura baada ya siku moja ili kuona iwapo litakaidi uamuzi wa bwana Trump , kulingana na kiongozi wa wengi katika chama cha Republican Mitch Connel. Lakin...

UBAGUZI WA RANGI TRUMP ASHUTUMIWA

Donald Trump ashutumiwa kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya wabunge wa Democratic Rashida Tlaib (kati), akiwa na Alexandria Ocasio-Cortez (kushoto) na Ayanna Pressley (kulia) Rais wa Marekani Donald Trump ameshutumiwa kwa ubaguzi wa rangu baada ya kundika ujumbe kwenye twitter akiwashambulia wabunge wanawake wa chama cha Democratic. Amedai kuwa wanawake hao "wamewasili kutoka mataifa ambayo serikali zake ni majanga matupu", kabla ya kupendekeza "warudi walikotoka". Baada ya hapo alisema kuwa spika Nancy Pelosi "atafurahi sana kuwashughulikia kwa haraka mipango ya safari ya bure". Haya ni wiki moja baada ya Bi Pelosi kukabiliana kwa maneno na "kundi hilo", la wabunge wasio watu weupe wa mrengo wa kushoto wa chama cha Democratic. Kati ya wabunge hao wanne, watatu - Alexandria Ocasio-Cortez, Rashida Tlaib na Ayanna Pressley - walizaliwa na kulelewa Marekani, huku wanne, Ilhan Omar, alihamia Marekani alipokuwa mtoto. Bi Ocasio-Cortez alizal...

Ripoti ya CAG yawasilishwa Bungeni Tanzania, asisitiza neno dhaifu ni la kawaida

Prof Mussa Assad ametiwa hatiani na Bunge kwa tuhuma za kudharau chombo hicho. Mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania Prof Mussa Assad amesisitiza kuwa ataendelea kutumia neno dhaifu. Akiongea na waandishi wa habari baada ya ripoti zake kuwasilishwa Bungeni, Prof Assad amesema neno hilo ni la kawaida kwenye fani ya uhasibu. "Neno 'dhaifu' naendelea kusisitiza ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. Na tutaendelea kulitumia," Prof Assad amesema. Hata hivyo Prof Assad hakuwepo Bungeni kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mkutano wake na wanahabari umefanyika kwenye ofisi yake mjini Dodoma. "Hatujakurupuka kufanya mkutano huu hapa ofisini kwetu. Tulihisi mapema hatutakaribishwa bungeni. Tumeongea nanyi hapa kwetu, hata kama ninyi waandishi wa habari hamtatoa hiki tulichozungumza, sisi tutatoa kwa umma," amesema Prof Assad. Azam TV@azamtvtz “Kwa mwaka 2017 tulitoa mapendekezo 350, yaliyotekelezwa kwa ukamilifu ni mapendekezo 8...

Waziri wa Uingereza akosoa Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania

Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje wa Uingereza akosoa Sheria ya Vyama vya Siasa Tanzania  Waziri Kivuli wa Mambo ya nje wa Uingereza Liz McInnes aimeikosoa Sheria ya Vyama vya Siasa Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje wa Uingereza ameeleza kusikitishwa kwake na kupitishwa kwa sheria ya vyama vya siasa nchini Tanzania ambayo anadai inaminya vyama vya upinzani. Liz McInnes ambaye ni mbunge kupitia chama cha upinzani Labour amekaririwa na  mtandao wa chama chake akisema wapinzani inabidi waachiwe uhuru wao . ''Inasikitisha kusikia kuwa bunge la Tanzania limepitisha sheria ambayo inazuia vikali shughuli za kisiasa na kutoa mamlaka kwa msajili wa vyama vya siasa kuvifutia usajili vyama vya upinzani''. ''Wanasiasa wa upinzani wanapaswa kuwa na uhuru wa kuipa changamoto serikali na si kuhofia kufungwa kwa kutoa maoni yao ikizingatiwa kuwa kuna chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzji mkuu mwakani''. Mwanasiasa huyo ametahadharisha kuwa mat...

Mabadiliko baraza la mawaziri Tanzania: Magufuli amfuta kazi Mwigulu Nchemba, Zitto Kabwe na Pole Pole walumbana

Mwigulu Nchemba Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri chini ya kipindi cha mwaka mmoja Aliyeathirika na mabadiliko ya Rais Magufuli siku ya Jumapili ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Lameck Nchemba ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Mwigulu Nchemba alipata umaarufu kwa juhudi zake za kuzuia maandamano dhidi ya Rais Magufuli. Alinukuliwa akitishia kuwalemaza waandamanaji na ''kuwakamata hata watakaoandamana wakiwa nyumbani". Licha ya hapo awali kuhamishwa kutoka wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi, hadi wadhfa wake wa mwisho, Nchemba ameondolewa baada ya kuhudumu kwa miaka miwili katika baraza la Rais Magufuli. Mbunge huyo wa Iramba aliyechukua nafasi ya aliyekuwa waziri Charles Kitwanga, sasa atampisha mbunge mwenzake kutoka Jimbo la Mwibara, Kangi Alphaxard Lugola kujaza pengo hilo. Ruka ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe Lugola amepandishwa ...

“Samaki wana maumbile kama Binadamu”- Musukuma

Mbunge wa Geita vijijini (CCM), Joseph Musukuma amesema kuwa samaki wako wa aina tofauti Ziwani na wengine wana tabia kama binadamu kwa kile alichodai wana maumbile madogo lakini wana umri mkubwa. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma akichangia Bungeni Musukuma ametoa kauli hiyo bungeni leo, wakati akihoji swali la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu kwa wizara ya mifugo na uvuvi ambapo amesema kuwa suala la kupima kwa rula samaki haliafiki kwa kuwa viumbe hao pia wana maumbile tofauti kama binadamu. “ Dhana ya uvuvi haramu imeenea sana, lakini samaki pia wana maumbile tofauti kama binadamu na mfano ukichukua umri wangu mimi na mheshimiwa Mwalongo tunalingana lakini ukitutazama maumbile tunatofautiana sana, sasa hata samaki wako hivyo, kwahiyo hata samaki wakipimwa kwa rula hawalingani, sheria haijalitazama hilo, Je ni lini sheria itamtazama mvuvi na kumlinda pindi anapokumbana na changamoto hii ya samaki kuwa na maumbile tofauti na umri wake ?”,...

Ndugai awachimba mkwara Wabunge wa 'hapana'

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewatahadharisha Wabunge wake kwamba endapo wataipigia kura ya hapana Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, Rais atalivunja Bunge hilo huku akiwakumbusha wengine wanaweza wasirudi kwenye mjengo huo. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo wakati akiwakumbusha wabunge kazi waliyonayo leo itakapofika saa 11 jioni  ambayo itakuwa kupiga kura ya kuipitisha bajeti. “Endapo mlio wengi mtaikataa Bajeti ya Serikali, bunge hili Rais atalivunja haraka. Na baadhi yenu, mkirudishwa majimboni hamrudi kwa hiyo akili za kuambiwa changanya na zako .” amesema Spika Ndugai. B Mbali na hayo Ndugai amewasisitiza wabunge wote kuwapo bungeni ifikapo saa 11  na kuwakumbusha kuwa kura haipigwi kwa jambo moja, bali ni kwa mfuko wote wa bajeti. Wabunge wanatarajia kupigia kura bajeti ambapo Serikali inatarajia kukusanya na kutumia TSh32...

Tundu Lissu awazuia wabunge

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amefunguka na kuwataka Wabunge wenzake bila ya kujali itikadi ya vyama vyao kutoshiriki kwenye hafla ya kupokea na kukabidhi taarifa za kamati maalum za kuchunguza na kushauri sekta ya Uvuvi wa bahari kuu na Gesi asilia iliyopangwa kufanyika kesho.  Lissu ametoa kauli hiyo mchana wa leo kupitia ukurasa wake wa kijamii mara baada ya Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuutarifu umma kuwa Juni 2, 2018 Spika wa Bunge Job Ndugai atapokea ripoti hizo ambazo zimepangwa kufanyikia katika viwanja vya Bunge mbele ya lango kuu la kuingilia. Kutokana na hilo, Lissu amedai kitendo hicho ni kinyume na zinaharibu taratibu za kisheria kwa kuwa taarifa za uchunguzi za Bunge huwa zinawasilishwa bungeni tena mbele ya wabunge wote na kujadiliwa endapo itahitajika kabla ya kukabidhiwa serikalini. "Nawaomba Wabunge wasikubali kushiriki katika maziko haya ya mamlaka ya kikatiba na kikanuni ya Bunge. Wadai taarifa hizi ziwasilishwe kwanza b...

"Wabunge hawafuati utaratibu"- Pius Msekwa

Sakata la matibabu ya Wabunge, Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa Wabunge hawafuati utaratibu kwa kufanya maamuzi yao binafsi. Msekwa amefunguka hayo wakati akizungumza na eatv.tv na kusema kuwa kuna taratibu za matibabu kwa Wabunge na hairuhusiwi kutibiwa hospitali yoyote kwa uamuzi binafsi lakini wanashindwa kufuata miongozo hiyo na kuibua migogoro. “Mbunge akiugua huwa anapelekwa hospitali ya serikali na endapo akitakiwa kuhamishwa hospitali atapewa rufaa na lazima bunge liwe na taarifa hakuna anayefanya maamuzi yake binafsi alafu anahitaji kulipwa”,  amesema Msekwa. Aidha, Msekwa ameongeza kuwa hakuna upendeleo kama ambavyo Kambi ya Upinzani Bungeni inavyodai na imekuwa hivyo tangu mwanzo kwa kuwa fedha zinazotumika ni za umma na zinataratibu zake. Hayo yamejiri baadaya kuwepo kwa madai kuwa Wabunge wa upinzani hawapewi kipaumbele pindi wanapotakiwa kupatiwa matibabu.

Mashambulizi dhidi ya Syria hayakuwa halali-Ripoti ya Bunge la Ujerumani

Ripoti ya wataalamu wa masuala ya sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani imesema mashambulizi yaliyofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Syria mapema mwezi Aprili yalikiuka sheria ya kimataifa. Ripoti ya wataalamu wa sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani, imesema mashambulizi yaliyofanywa na nchi tatu za Magharibi hayakuwa halali kisheria. Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliishambulia Syria kwa makombora tarehe 14 Aprili, kwa madai kwamba zilikuwa zikiiadhibu serikali ya Rais Bashar al-Assad, ziliyemshutumu kutumia gesi ya sumu kuwashambulia raia katika mji wa Douma. ''Matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya nchi huru, kama hatua dhidi ya ukiukaji wa sheria na kanuni za kimataifa unaodaiwa kufanywa na nchi inayoshambuliwa, ni uvunjaji a sheria ya kimataifa inayozuia matumizi ya ghasia,'' imesema ripoti hiyo ya wataalamu wa kisheria wa Bunge la Ujerumani, Bundestag. Ripoti hiyo iliombwa na chama cha mrengo wa kushoto (Die-Linke) cha Uj...

Wizi wa almasi: Mugabe atakiwa kutoa ushahidi

Bunge la Zimbabwe limemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi. Bunge la Zimbabwe limemtaka rais wa zamani wa taifa hilo Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi. Bwana Mugabe alizishutumu kampuni za kigeni za kuchimba madini kwa ''kuiba'' na ''kusafirisha'' katika mahojiano na runinga ya taifa 2016. ''Kampuni hizo zimetuibia utajiri wetu'' , alisema. Akiongzea kuwa wizara ya fedha ilipokea $15bn pekee. Haijulikani iwapo raia huyo mwenye umri wa miaka 94 atakubali kufika mbele ya kamati hiyo ya bunge. Alilazimishwa kujiuzulu mwezi Disemba iliopita kufuatia mapinduzi ya kijeshi na bado anahudumiwa na serikali kama rais wa zamani