Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamesema watawatumia wabunge kumi na tisa wa chama hicho kulinda kura katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kizota katika jiji la Dodoma. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea). Viongozi walitoa kauli hiyo jana nje ya ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kizota muda mfupi baada ya mgombea udiwani kata hiyo kupitia Chadema, Omar Bangababo kurejesha fomu ya ugombea kata hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wa Chadema Kanda ya Kati, Iddy Kizota amesema watawatumia wabunge wa Chadema kulinda kura za mgombea kutokana na kuwapo kwa hujuma za kuwapiga mawakala na kuwaondoa vituoni kwa lengo la kubadilisha matokeo. Hata hivyo Kizota amesema kulikuwepo na njama kubwa ambazo zilikuwa zikifanywa na Ofisi Mtendaji wa Kata ya Kizota, Loyce Mrefu kwa kutaka kumkwamisha mgombea wa Chadema kwa kumwekea vikwazo visivyokuwa na sababu. “Unaweza kujiuliza msimamizi wa uchaguzi ...