Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UKAME

Ukame Kenya :Turkana County Serikali ya kili wananchi kufa kwa njaa

 Watu zaidi ya 10  wamefariki kutokana na uhaba wa chakula Turkana County  Zaidi ya watu 800,000 wanaendelea kuumia kwa makali ya njaa na kiu kwa mujibu wa wizara ya kudhibiti majanga na utumishi wa umma ya kaunti ya Turkana. BBC Huyu ni mama Audan Loteng' Takwa aliye na umri wa miaka 63. Anaelezea masaibu anayopitia yeye na wanakijiji wenzake ambao wanahofia huenda wakaangamia kwa njaa iki serikali ya Kenya haitaingilia kati hali yao. BBC Anna Emaret anasema amekuwa akigawana chakula na mifugo wake, lakini chakula kilipoisha, wakafa. BBC Mama huyu ana ujauzito wa miezi sita na hajakula chochoto kwa siku tatu zilizopita. BBC Mariam Loolio ni ajuza mwenye umri was miaka 85. Kwa siku tano anasema hajala chochote. BBC Kwa mujibu wa mtazamo kuhusu uwepo wa chakula cha kutosha kwa Kenya 2019 , baadhi ya maeneo ya mashariki, kaskazini na kaskazini magharibi mwa Kenya ambapo kuna jamii za wafugaji, huenda zikakabiliwa na mzozo wa uhaba wa chakula. ...

Kenya: Raia watumia mitandao ya kijamii kuitaka serikali iwajibike na baa la njaa

Wazee, watoto, wanawake wajawazito na watu wenye ulemavu wanaendelea kuumia kutokana na ukosefu wa chakula na maji. Huku Wakenya wakiendelea kujadili haja ya serikali kushughulikia ukame, makali ya njaa yanaendelea kushuhudiwa katika kaunti ya Turkana ambayo imekumbwa na ukame. Chini ya #WeCannotIgnore , Wakenya kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa wakiitaka serikali ichukua hatua juu ya njaa inayoendelea kusababisha vifo . Mjadala huo unaendelea huku idadi ya watu waliokufa kutokana na njaa ikipanda ambapo shule zimelazimika kufungwa huku wanafunzi wakiwafuata wazazi wao kwenye maeneo ya misitu kutafuta chakula. Hakimiliki ya Picha @NyangePatience@NYANGEPATIENCE Wakenya wanauliza 'Ni nini kilitokea kwa mfumo unaotoa taarifa za mapema za maafa?' na kwanini Wakenya wanakabiliana na njaa, katika nchi ambayo usalama wa chakula imekuwa ndio ajenda inayopewa kipaubele zaidi?. Hakimiliki ya Picha @JamilaMohamed@JAMILAMOHAMED Wazee, watoto, wanawake wajawazito na watu we...