Michael Job, mhubiri wa Marekani na muigizaji ambaye hivi majuzi alizuru Kenya na kuitwa 'Yesu bandia' hajafariki kama ilivyoangaziwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania na Kenya. Kulingana na uchunguzi wetu jamaa huyo yupo hai na mzima wa afya. Kadhalika, mhubiri huyo yupo nchini Kenya na kwamba hajatimuliwa kama ilivyodaiwa na vyombo hivyo vya habari. Taarifa za vyombo hivyo ambazo zilianza kuenezwa siku tano zilizopita zinadai, Yesu huyo bandia alifariki siku chache tu baada ya kuhudhuria ibada ya kidini. Mwisho wa ujumbe wa Facebook wa Michael Inadaiwa kwamba alifariki siku chache tu baada ya kutembelea taifa hilo la Afrika mashariki baada ya kuuguwa ugonjwa wa mapafu. Hata hivyo mhubiri huyo ameendelea kupakia mtandaoni picha na video ya shughuli zake siku baada ya siku. Picha na video za karibuni zaidi alizipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook saa nne usiku wa kuamkia leo. Katika chapisho hilo na kanda za video alizoweka katika akaunti...