Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WIZARA YA AFYA

MPANGO WA KUIMARISHA UBORA WA AFYA NA USTAWI WA WATOTO NI NYENZO MUHIMU- DKT. SHEKALAGHE

Picha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amesema Mpango wa Kuimarisha Ubora wa Afya na Ustawi wa Watoto ni nyenzo muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watoto na vijana nchini. Dkt. Shekalaghe amesema hayo leo Julai 23, 2025 mkoani Arusha wakati wa kongamano la Pili la Kitaifa la Afya na Ustawi wa Watoto baada ya kuzindua rasmi mpango huo wenye lengo la kushughulikia changamoto zinazowakabili watoto na vijana ikiwemo matatizo ya lishe, mimba za utotoni na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU). Mpango huo umeandaliwa na Chama cha Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania (Pediatric Association of Tanzania – PAT) kwa kipindi cha miaka Mitano (5) kuanzia mwaka 2025 hadi 2030 ambao umejikita katika kushughulikia vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ya kiafya kwa watoto na vijana, hasa wenye umri wa miaka 15-19. Vipaumbele vya mpango huo ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Wizara ya Afya na wadau wa sekta ya afya, kushawishi na kuandaa sera zitakazosaidia ...

MAPACHA WATANZANIA WALIOUNGANA WATENGANISHWA

Picha
  MAPACHA wa Tanzania walioungana, Anishia na Melanese, wametenganishwa nchini Saudi Arabia Desemba 23, 2018, na hali zao zinaendelea vizuri kwa wakati huu.   Jumanne Desemba 25, 2018 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha amethibitisha mapacha hao kutenganishwa.   Kwa mujibu wa gazeti la nchini Saudi Arabia, saudigazette.com mapacha hao walitenganishwa na jopo la wataalamu 32 kwa muda wa saa 13.   Upasuaji huo uliofanyika katika hospitali ya Mfalme Abdullah, (King Abdullah Children’s Specialist Hospital) iliyopo katika mji wa Riyadh (King Abdulaziz Medical City), uliongozwa na Dk Abdullah Al-Rabeeah.   Mapacha hao wa kike waliozaliwa katika Kituo cha Afya cha Missenyi, Kagera, Januari 2018,  walipofikishwa Saudi Arabia walifanyiwa vipimo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya kuona uwezekano wa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha