Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KITAIFA

TANZANIA YAUNGA MKONO UHURU WA CHAKULA KATIKA MKUTANO WA UNFSS+4 JIJINI ADDIS ABABA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri uliofanyika tarehe 29 Julai 2025, jijini Addis Ababa, Ethiopia, uliokuwa sehemu ya Mkutano wa Pili wa Mfumo wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (UNFSS+4). Katika hotuba yake kwenye majadiliano ya Meza ya Mawaziri kuhusu Uhuru wa Chakula na Njia za Kitaifa katika Kuharakisha Mageuzi ya Mifumo ya Chakula, Mhe. Kombo amesisitiza msimamo wa Tanzania wa kuunga mkono dhana ya uhuru wa chakula (food sovereignty), akisema ni haki ya jamii kuamua namna bora ya kuzalisha, kusambaza na kutumia chakula kulingana na mahitaji, tamaduni na vipaumbele vyao. Amesema kwa Tanzania, uhuru wa chakula si ndoto ya muda mrefu bali ni sharti la msingi kwa ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho, hasa ikizingatiwa changamoto za mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa bei za chakula, upotevu wa mazao baada ya mavuno na usumbufu katika minyororo ya usambazaji ya ...

Waziri Mkuu wa Ufaransa akosoa makubaliano ya biashara ya EU 'kuwasilisha'

Waziri Mkuu wa Ufaransa akosoa makubaliano ya biashara ya EU 'kuwasilisha' Mkataba mpya uliotiwa saini unawakilisha "siku ya giza" kwa Uropa, Francois Bayrou amesema Waziri Mkuu wa Ufaransa akosoa makubaliano ya biashara ya EU 'kuwasilisha' Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Bayrou akitoa hotuba mjini Paris, Ufaransa, Julai 15, 2025. © Getty Images / Ameer Alhalbi Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Bayrou amelaani makubaliano mapya ya kibiashara kati ya Washington na Brussels, akishutumu Umoja wa Ulaya kwa kukubali kulazimishwa na Marekani. Siku ya Jumapili, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alikamilisha makubaliano yenye utata na Rais Donald Trump, na kuepusha kutoza ushuru wa 30% kutoka kwa Marekani badala ya ushuru wa 15% kwa bidhaa nyingi. Kwa upande wake, EU ilikubali kufungua masoko yake kwa mauzo ya nje ya Marekani na kutowatoza ushuru. "Mkataba wa Von der Leyen-Trump: Ni siku ya giza wakati muungano wa watu huru, waliokusanyika...

BALOZI DKT. NCHIMBI AZUNGUMZA NA DKT. MPANGO

Picha
BALOZI DKT. NCHIMBI AZUNGUMZA NA DKT. MPANGO Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi alizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdory Mpango, baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa.  Mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ulifanyika kwa njia ya mtandao katika Ukumbi wa Mikutano wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Jumamosi tarehe 26 Julai 2025, jijini Dodoma. Aidha, wanaoonekana katika picha ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ambao ni, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (kulia) pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe Zubeir Ali Maulid.