Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UCHAGUZI MKUU

KATIBA YA CCM YARUHUSU MIKUTANO YAKE KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO

Picha
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, kufanya mabadiliko madogo ya Katiba ya CCM ambapo sasa Katiba hiyo inatambua ufanywaji wa mikutano ya ngazi mbalimbali kwa njia ya mtandao maarufu kama E- Meeting. Kulingana na Dkt. Samia wakati akitangaza mapendekezo hayo kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Mabadiliko hayo ni katika kuhakikisha kuwa Chama hicho kinaenda sawa na mabadiliko mbalimbali ya teknolojia yanayotokea duniani,suala ambalo limewezesha CCM pia kufunga Mitambo ya teknolojia yenye kuwezesha Ngazi za CCM wilaya na Mikoa kuweza kuunganishwa pamoja na Makao Makuu kwa njia ya mtandao. Rais Samia amebainisha kuwa Idara ya Oganaizesheni ilipendekeza vikao vitakavyoweza kufanyika kimtandao ni Vikao vya Sekretarieti ya Wilaya, Kamati za siasa za wilaya, Sekretarieti za Mikoa, Kamati za siasa za Mikoa, sekretarieti ya Kamati maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kamati ...

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha majimbo mapya nane na kubadilisha majina ya majimbo 12 ya uchaguzi

Picha
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha majimbo mapya nane na kubadilisha majina ya majimbo 12 ya uchaguzi yatakayotumika kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 12 Mei, 2025 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amesema Tume imefikia uamuzi huo baada ya kupitia maombi kutoka kwenye mikoa mbalimbali nchini. Amesema uamuzi huo umefanyika kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 75(1), (2) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kanuni ya 18(7) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024. Ameyataja majimbo hayo kuwa ni Jimbo la Kivule amabalo limegawanywa kutoka Jimbo la Ukonga na Jimbo la Uchaguzi la Chamanzi ambalo limegawanywa kutoka Jimbo la Mbagala yote ya mkoani Dar es Salaam. “Mkoani Dodoma limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la Dodoma Mjini limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la ...