Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi? Sehemu mbalimbali duniani mtazamo kuhusiana na matumizi ya mmea wa cannabis yaani bangi unabadilika kwa kasi. Serikali mpya ya Mexico ina mpango wa kuhalalisha matumizi ya bangi kama njia ya kujiburudisha, sawa na ilivyofanya utawala mpya wa Luxembourg. Wakati huo huo, viongozi wakuu nchini New Zealand, wanakusudia kuandaa kura ya maoni ya namna watakavyoshughulikia swala hilo. Jinsi maoni ya umma - na yale ya serikali- yanavyobadilika, ni dhahiri kuwa mataifa mengi yatafuata mkondo huo. Maswali yanayoibuka ni kwa namna gani nchi hizo zitadhibiti matumizi na usambazaji wa mmea huo? Ni nini hasa kinachopelekea mataifa mbalimbali katika kulegeza kamba kwenye sheria zake, au hata kuamua kuidhinisha ,matumizi ya bangi moja kwa moja? Vita dhidi ya mihadarati Ilikuwa mwaka 2012 ambapo Uruguay, ilipoandika historia kwa kuwa taifa la kwanza duniani kuruhusu matumizi ya bangi kwa minajili ya kujiburudisha. Hatua hiyo, ...