MTEULE THE BEST Upinzani nchini Venezuela umeahidi kuendelea kumshinikiza rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro, baada ya maelfu ya waandamanaji kumiminika majiani katika mji mkuu wa Caracas hapo jana Waandamanaji hao wanataka kuitishwe kura ya maoni ya kumuondoa madarakani kiongozi huyo, kabla ya Januari 10. Iwapo Maduro atashindwa katika kura hiyo ya maoni, italazimika kufanyike uchaguzi wa mapema. Kiongozi wa upinzani wa chama cha Democratic Unity Roundtable, Jesus Torrealba, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba yalikuwa ni maandamano makubwa kuwahi kutokea katika miongo kadhaa iliyopita. Alisema kuwa kati ya watu 950,000 hadi milioni moja na laki moja walijitokeza katika maandamano hayo. Na wameahidi kuendelea na shinikizo hilo hadi pale rais wa nchi, Nicolas Maduro, "Leo ndiyo mwanzo wa jitihada zetu tukiwa pamoja na raia wote wa Venezuela, wanaotimiza haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa amani hadi pale kutakapopatikana mabadiliko ya kikatiba na yaliyo...