Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MAASKOFU

Kujikabidhi kwa Yule anayeongoza Kanisa

Picha
2025.05.08 Uchaguzi wa Papa wa ROma.  (@Vatican Media) Mwariri mkuu wa Baraza la kipapa la Mawasiliano kwa mtazamo wa kuchaguliwa kwa Papa mpya ambaye amebainisha:“Leo hii ulimwengu uko katikati ya dhoruba,inayotikiswa na vita na jeuri.Tuombe amani.Tuombe pamoja na Petro na Petro ambaye leo hii alichukua jina la Leo,akiungana tena na Papa wa Waraka wa kitume wa “Rerum novarum.” Andrea Tornielli Jimbo la Roma lina Askofu wake, Kanisa la ulimwengu wote lina mchungaji wake. Kwa kasi ambayo inaweza  kuwashangaza tu wale wanaosoma maisha ya Kanisa kupitia lenzi za siasa, Mkutano Mkuu umemteua Mrithi wa Petro. Asante, Baba Mtakatifu, kwa kukubali. Asante kwa kusema "ndiyo" na kwa kujiacha kwa Yeye anayeongoza Kanisa. Maneno ya kukumbukwa yaliyosemwa na Paulo VI mbele ya wanafunzi wa Chuo cha Lombardia , mnamo Desemba 1968, wakati wa kipindi kigumu cha kupinga katika kipindi cha baada ya mtaguso, yanakumbuka tena: “Wengi - alisema Papa - wanatarajia kutoka kwa Papa ishara za hisia, ...

PAPA FRANCISCO NA MAPADRE WATANZANIA & CDF MABEYO

Picha
▪︎Katika picha ni Papa Francisco akiwa na Mapadre watanzania wanaosoma na kufanya utume wako nchini Italia pamoja Na Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. ▪︎Ikumbukwe Maaskofu wote nchini Tanzania wako katika ziara ya Kichungaji yalipo makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani mjini Vatican tangu May 14 hadi May 21, 2023. ▪︎Pia katika ziara hiyo wameambatana na Mapadre kadhaa akiwemo Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padre Chesco Msaga C.PP.S Naibu Katibu Mkuu (TEC) bila kumsahau Padre Thomas Kiangio Msimamizi  wa Jimbo Katoliki Tanga. . . RADIO MARIA TANZANIA