Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 16, 2017

Morata kusajiliwa Chelsea

MTEULE THE BEST Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano na mabingwa wa Ligi kuu ya Hispania (La Liga), Real Madrid kuhusiana na uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Alvaro Morata. Inaelezwa kuwa uhamisho wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 umegharimu takribani dola za kimarekani million 78 ambazo ni sawa na pauni milioni 60 za Uingereza. Mapema leo, mchezaji huyo ambaye ni zao halisi la Real Madrid, ameagana na wachezaji wenzake wa Real Madrid akiwemo kocha Zinedine. The Blues waliamua kuhamishia majeshi kwa Morata baada ya chaguo lao la awali Romelu Lukaku kuamua kuungana na Jose Mourinho katika kikosi chake cha Manchester United. United na wenyewe walitajwa kumuhitaji Morata lakini walilazimika kugeukia wa Lukaku baada ya kushindwa kufikia dau lilotajwa kuwa ni dola za kimarekani milioni 97.

TTCL PESA YAZINDULIWA NA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA

MTEULE THE BEST Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL Pesa uliofanyika Makamu Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.   Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba akimuonesha namna ya kutumia huduma ya TTCL Pesa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa TTCL Pesa uliofanyika Makamo Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar Es Salaam.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua huduma mpya ya fedha mtandao ijulikanayo kama TTCL PESA ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL. Uzinduzi huo umefanyika katika Makao Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Omari Nundu ambaye ni Mwenyeketi wa Bodi ya TTCL, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujezi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete, Afisa Mtendaji Mkuu w...

TRA:HATUMTAMBUI NGELEJA

MTEULE THE BEST Waziri wa Nishati na Madini wa zamani Ngeleja ni mmoja kati ya watu waliopokea mgawo wa fedha zinazodaiwa kuwa zao la kashfa ya Tegeta Escrow, lakini akatangaza kuzirejesha kwa TRA Jumatatu iliyopita.  Februari 2014, Ngeleja ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Sengerema (CCM) aligaiwa Sh. milioni 40.4 na mfanyabiashara maarufu James Rugemalira ambaye mwanzoni mwa mwezi alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka 12, yakiwamo ya kughushi na utakatishaji fedha.  Hata hivyo, wakati Ngeleja akithibitisha kwa risiti mbele ya waandishi wa habari kuziingiza fedha hizo katika akaunti ya TRA, mamlaka hiyo imesema haizitambui. TRA imesema haina mpango wowote wa kufuatilia fedha hizo kwa sababu shughuli yake ni kukusanya kodi.  Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo inahusika na kuhakikisha serikali inakusanya kodi stahiki na siyo urejeshaji wa fedha za kashfa kama Escrow.  Kayombo ...