Takriban watu 20 wamefariki dunia na wengine 48 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha zaidi ya magari matatu mkoani Mbeya, kanda ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Ajali hiyo ilitokea katika mteremko wa Iwambi mkoani Mbeya. Hii ni ajali ya tatu kutokea Mbeya katika kipindi kifupi ambapo katika ajali hizo idadi ya Watanzania waliopoteza maisha imefikia 40. Mnamo 14 Juni, watu 13 wakiwemo vijana 11 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), askari 1 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na dereva walipoteza maisha, na jumla ya watu 25 wakajeruhiwa, majira ya mchana baada ya ajali kutoka katika mteremko wa Mwansekwa uliopo Mjini Mbeya. Aprili, watu wanane waliokuwa kwenye gari ndogo aina ya Toyota Noah walifariki dunia papo hapo baada ya gari hilo kugongana uso kwa uso na basi katika eneo la Igodima. Gari hilo lililokuwa likitokea Chunya kwenda Mbeya mjini, lilikuwa na abiria tisa waliokuwa wakienda katika msiba wa ndugu yao. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoan...