Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UPELELEZI

Kitambulisho cha Vladimir Putin akiwa jasusi wa KGB chapatikana Ujerumani

Vladimir Putin alikuwa na umri wa miaka 33 alipopewa kitambulisho hicho Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini Dresden. Rais huyo wa Urusi amekuwa mara kwa mara akisema anajivunia kazi aliyoifanya akiwa kama jasusi wa idara ya ujasusi ya Urusi wakati huo ikifahamika kama KGB jijini Dresden miaka ya 1980. KGB kwa kirefu ni Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti (Kamati/Idara ya Usalama wa Taifa) Putin, wakati huo, alipewa kitambulisho na idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Muungano wa Usovieti (USSR). Idara ya ujasusi ya Ujerumani Mashariki ilifahamika kama Stasi, lakini kwa kirefu ni Ministerium für Staatsicherheit kwa maana ya maajenti wa Wizara ya Usalama wa Taifa. Kitambulisho cha Stasi alichokitumia Putin kimegunduliwa wakati wa uchunguzi kuhusu ushirikiano wa karibu uliokuwepo kati ya KGB na Stasi. Putin ambaye wakati huo...