Picha mpya za falaki yetu ya Milky Way Mfumo wetu wa sayari na nyota, ama falaki, upo katika umbo la upinde na si nyoofu kama ilivyodhaniwa hapo awali, utafiti mpya umebaini. Njia hiyo ya falaki, maarufu kwa lugha ya Kiingereza kama Milky Way, katika vitabu vyote vya sayansi na taaluma inaoneshwa ipo katika unyoofu. Hata hivyo, utafifiti mpya wa nyota zing'aazo zaidi kwenye falaki hiyo umebaini kuwa nyota hizo hazipo kwenye njia nyoofu, zimepinda. Wataalamu wa unajimu kutoka Chuo Kikuu cha Warsaw wanadhani kuwa nyota hizo zimepinda kutoka kwenye njia nyoofu ikiwa ni matokeo ya kutangamana na falaki nyengine za karibu. Ramani mpya tatu za falaki ya Milky Way zimechapishwa kwennye jarida la Science . Picha maarufu zaidi ya Milky Way ikiwa katika mstari nyoofu imetokana na utafiti wa nyota milioni 2.5 kati ya nyota zipatazo bilioni 2.5 katika falaki hiyo. Dr University. "Undani wa kimfumo na historia ya falaki ya Milky Way bado kabisa kujulikana, na moja ya saba...