Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 3, 2017

Gwiji wa muziki wa country Don Williams afariki dunia

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Don Williams alianza kuimba muziki kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971 Mwanamuziki nyota wa nyimbo za mtindo wa country kutoka Marekani Don Williams amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78. Mzaliwa huyo wa jimbo la Texas amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi, afisa anayesimamia mawasiliano yake ametangaza. Williams alianza kuimba nyimbo kama mwanamuziki wa kujitegemea mwaka 1971, na tangu wakati huo alichomoa nyimbo 17 zilizogonga chati za muziki wa country. Nyimbo zake zilizovuma zaidi ni pamoja na  Gypsy Woman  na  Tulsa Time , ambazo ziliimbwa tena na wanamuziki wengine kama vile Eric Clapton na Pete Townshend. Williams alitazamwa na wengi kama gwiji mnyenyekevu wa muziki wa country. Nyimbo zake nyingine zilizovuma ni pamoja na  You're My Best Friend, I Believe in You  na  Lord, I Hope This Day Is Good . Haki miliki ya picha GETT...

Marekani yataka mali ya Kim Jong-un kutwaliwa

MTEULE THE BEST Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha KCNA Image caption Marekani yataka kutwaliwa mali ya Kim Jong-un Marekani imendekeza vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwemo marufuku kwa biashara ya mafuta na kutwaliwa kwa mali ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. Azimio lililowasilishwa kwa wanachama wa baraza la ulinzi wa Umoja wa Mataifa, linakuja baada ya jaribio la sita la nyuklia kufanywa na Korea Kaskazini. Korea Kaskazini inadai kuunda bomu la haidrojeni na imekwua ikitishia kuishambulia Marekani. Korea Kusini yafanya majaribio ya makombora kujibu majaribio ya Korea Kaskazini Bomu la Korea Kaskazini: Tunayoyajua kufikia sasa China na Urusi zote zinatarajiwa kupinga vikwazo zaidi. Korea Kaskazini tayari iko chini cha vikwazo vya kuitenga vilivyotangazwa na Umoja wa Mataifa, ambavyo vina nia ya kuulazimisha utawala wa nchi hiyo kusitisha mipango yake ya nyuklia. Mwezi Agosti vikwazo vipya vya Umoja wa Ma...

Magazeti ya Tanzania leo September 7 2017 kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa

MTEULE THE BEST Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo September 7  2017  kuanzia ya Udaku, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.

Papa Francis kuwasili Colombia kwa ziara ya siku tano

MTEULE THE BEST Image caption Ni ziara ya kwanza ya Papa nchini Colombia ndani ya kipindi cha miongo mitatu Papa Francis anatarajiwa kuwasili mji mkuu wa Colombia, Bogota saa chache kutoka hivi sasa, ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na Papa nchini humo ndani ya miongo mitatu. Katika ziara yake ya siku tano, anatarajiwa kugusia mazungumzo ya amani yaliyofikiwa mwaka jana kati ya serikali na kikosi cha waasi cha Farc. Image caption Rais Juan Manuel Santos anasema ujio wa Papa ni ishara kwamba nchi hiyo inapenda amani Kuelekea ziara hiyo, waasi wa ELN ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo, wamekubali kuweka silaha chini kwa muda na kufanya mazungumzo ya amani,tukio ambali Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ameliita ni miujiza kabla ya ujio wa Papa.

Chama cha Kenyatta chapinga maafisa wapya wa uchaguzi Kenya

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha UHURU KENYATTA/TWITTER Image caption Bw Kenyatta na naibu wake William Ruto Chama cha Jubilee, chake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kimepinga kundi la maafisa tisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya mwezi ujao. Chama hicho kimetoa orodha ya majina ya maafisa hao ambao kinasema wanajulikana kwamba "wanapendelea upande fulani". Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC alitangaza kundi la maafisa saba watakaoongoza maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 17 Oktoba siku ya Jumanne. Maafisa hao ambao wanajumuisha mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) na msimamizi wa kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo watahudumu kwa miezi mitatu. Odinga apinga tarehe mpya ya uchaguzi Kenya Rais Kenyatta: Ni haki yangu kuikosoa mahakama Chama cha mawakili Kenya chamkosoa Uhuru Kenyatta Mahakama ya Juu, ikifutilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti ambapo...

KENYA: Al Shabaab wawakata shingo watu 4

MTEULE THE BEST Polisi nchini Kenya wanasema raia waiopungua wanne wameuawa kwa kukatwa shingo na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la al Shabaab lenye makao yake katika nchi jirani ya Somalia. Mkuu wa polisi wa Pwani ya Kenya, Larry Krieng, amesema shambulio hilo lilifanyika siku ya Jumatano (Septemba 6) asubuhi katika eneo la Bobo, kijiji cha Hindi, Kaunti ya Lamu. Shambulio hilo linapelekea idadi ya watu walioripotiwa kuuawa kwa kukatwa shingo na wafuasi wa al Shabaab katika Kaunti hiyo kuwa 16 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Mauaji ya kukatwa shingo yalikuwa jambo la nadra nchini Kenya lakini ni ya kawaida nchini Somalia, ambako wafuasi hao wa itikadi kali wanayatumia kueneza hofu miongoni mwa wakaazi. Al Shabaab imeapa kuiadhibu Kenya kwa hatua yake ya kutuma vikosi nchini Somalia kupambana na kundi hilo. Kundi hilo limefanya mashambulizi kadhaa nchini Kenya tangu mwaka 2011, lakini mashambulizi ya karibuni yamejikita zaidi katika kaunt...

04/9/2017 Lil Wayne alazwa hospitalini kwa kuugua kifafa

MTEULE THE BEST Image caption Mwanamuziki wa nyimbo za kufoka Lil Wayne Mwanamuziki Lil Wayne amekimbizwa hospitalini baada ya kuanguka kutokana na kifafa na kupatikana akiwa hana fahamu katika chumba cha hoteli alimokuwa huko Chicago. Mtandao wa wasanii wa TMZ umesema mwanamuziki huyo wa nyimbo za kufoka, 34, anayeugua ugonjwa wa kifafa, ameangushwa na ugonjwa huo mara kadhaa na alipoteza fahamu pindi tu alipowasili huko A&E. Alitarajiwa kuwatumbuiza mashabiki wake huko Las Vegas siku ya Jumapili usiku. Nyota huyo, ambaye kwa jina lake rasmi Dwayne Michael Carter Jr, alipokea matibabu mwaka uliopita baada ya kupoteza fahamu mara mbili lakini kwa kiasi kidogo. Miaka minne iliyopita Lil Wayne alikuwa akipokea matibabu kwa siku kadhaa katika hospitali moja huko Los Angeles. Baada ya kupata fahamu, mwanamuziki huyo aliambia kituo cha redio cha Power 106 kwamba, anaugua ugonjwa wa kifafa na yuko katika hatari za kukosa fahamu mara kadhaa. Alimwambia DJ Felli Fel: ...

Bomu la Korea Kaskazini lilisababisha 'maporomoko ya ardhi'

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha PLANET / 38 NORTH Image caption Picha za 38 North zinaonesha maporomoko kadha yaliyokea karibu na kilele cha Mlima Mantap Majaribio ya bomu la nyuklia ambayo yalifanywa na Korea Kaskazini Jumapili yalisababisha maporomoko kadha ya ardhi, kwa mujibu wa picha za setilaiti ambazo zinaaminika kuwa za kwanza kabisa za eneo ambalo majaribio hayo yalifanyika. Majaribio hayo ya bomu yalifanyika chini ya ardhi katika eneo la kufanyia majaribio silaha linalotumiwa na Korea Kaskazini la Punggye-ri ambalo lina milima mingi. Kundi la uchunguzi kwa jina 38 North limechapisha picha ambazo zinaonekana kuonyesha "maporomoko kadha katika eneo kubwa" kuliko yaliyowahi kushuhudiwa awali. Mlipuko wa bomu hilo ulisababisha tetemeko la ardhi la nguvu ya 6.3 kwenye vipimo vya Richter. Tetemeko hilo lilisikika hadi China na katika baadhi ya maeneo ya Urusi. Korea Kaskazini imefanya majaribio sita ya silaha za nyuklia kufikia sasa, yote katika eneo...