MTEULE THE BEST Rais wa Marekani Donald Trump ameutaja utawala wa taifa la Korea Kaskazini kuwa wa kikatili kufuatia kifo cha mwanafunzi mmoja wa Marekani ambaye alikuwa amefungwa jela kwa zaidi ya miezi 15 nchini humo. Korea Kaskazini ilimrudisha nyumbani Marekani, Otto Warmbier mwenye umri wa miaka 22 wiki iliopita ikisema kuwa alikuwa hana fahamu kwa kipindi cha mwaka mmoja na kwamba ilikuwa ikimsaidia kibinaadamu. Wazazi wake wanasema kuwa aliteswa vibaya. Otto Warmbier aaga dunia Korea Kaskazini yamwachilia huru Mmarekani Mwanafunzi aliyeachiliwa na Korea Kaskazini alazwa hospitalini Korea: Tulimwachilia mwanafunzi kwa misingi ya kibinadamu Bwana Warmbier ambaye alifungwa kwa kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwa hoteli moja hakuweza kupata fahamu tena. Haki miliki ya picha EPA Image caption Otto Warmbier alipokamatwa baada ya kujaribu kuiba bango la propaganda Bwana Trump alisema kuwa kifo cha Warmbier kimeimarisha mipango ya utawala wake wa kutaka...