Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya AJARI

Waabiri ndege kisiri 'stowaway' huponea?

Mshukiwa aliyeabiri ndege kisiri inaaminika ameanguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways  kutoka Nairobi kuelekea Heathrow, na kuanguka katika bustani moja huko kusini mwa London Lakini ni mara ngapi visa kama hivyo huhuhudiwa na hali huwa vipi wakati wa safari za aina hiyo? Ni mara ngapi visa hivi hutokea? Licha ya kwamba sio jambo la kawaida, hii sio mara ya kwanza kwa mtu kuingia katika sehemu za ndege wakati ndege hiyo ikisafiri na kujificha wakati wa safari ya kuelekea Uingereza. mwili ulipatikana katika bustani ilioko Offerton Road huko Clapham Kati ya Januari 2004 na Machi 2015, watu sita walioingia kwa siri katika ndegekatika uwanja wa ndege Uingereza walipatikana kwa mujibu wa  takwimu za hivi karibuni za shirika la viwanja vya ndege (CAA ). Mwingine mmoja alipatikana katika ndnai ya ndege ya Uingereza katika uwanja wa ndege ng'ambo. Takwimu kutoka shirika la viwanja vya ndege Marekani zimeashiria kuwa watu 96 wamewahi kujificha katika sehemu za ndege ...

Tanzia: sita wafariki kwa ajali Morogoro

Watu sita wamefariki dunia kwa kwa ajali ya gari mkoani Morogoro, ambapo miongoni mwa waliofariki ni msanii maarufu wa muziki wa mchiriku na singeli kutoka kundi la 'Jagwa', Jack Simela. Ajali hiyo imetokea katika eneo la Msamvu mkoani Morogoro, baada ya gari lao dogo lililokuwa likitokea kwenye mazishi mkoani humo kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dkt. Simon Tarimo, amethibitisha kupokea miili sita na majeruhi wawili, na kusema kwamba hali za majeruhi zinaendelea vizuri hospitalini hapo. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijawekwa wazi, baada ya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro kugong mwamba. Jack Simela alikuwa ni muimbaji kiongozi wa kundi la Jagwa Music ambalo ni maarufu kwa muziki aina ya mchiriku, muziki ambao umekuwa ukipendwa na mataifa ya nje ikiwemo Ujerumani, ambako ndiko mara nyingi yeye na kundi lake walikuwa wakienda kufanya matamasha.         ...

Ndege mpya inawezaje kuanguka

Lion Air: Haki miliki ya pichaBOEINGImage captionNdege aina ya Boeing MAX 8 ilikuwa imehudumu chini ya mwaka mmoja Ndege ya shirika la Lion Air iliyoanguka baharini, ikiwa na abiria karibu 190 muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu wa Jakarta nchini Indonesia imeendelea kuvutia hisia mbali mbali. Ndege hiyo aina ya Boeng 737 MAX 8, ilikua mpya. Hii ni ajali ya kwanza kuhusisha ndege aina hiyo. Maelezo kuhusu nini hasa kilitokea yamekua finyu lakini chanzo cha ajali hiyo kitajulikana baaada ya uchunguzi kufanywa. Ajali ya ndege mara nyingi husababishwa na mchanganyiko wa mambo tofauti ikiwa ni pamoja na hitilafu ya kimitambo au makosa ya kibinadamu-lakini je ndege mpya inawezaje kuanguka? Ndege hiyo ya Boeng 737 MAX 8 iliyohusika katika ajali siku ya jumatatu ilikuwa imehudumu kutoka mwaka Agosti 15 mwaka 2017 Kwa mujibu wa mkuu wa tume ya kitaifa ya usalama wa uchukuzi wa angani Soerjanto Tjahjano ndege hiyo ilikua imesafiri kwa saa 800. Inasemekana rubani aliomba w...

Watu 10 wafa kwa kugongwa na gari kimakusudi nchini Canada

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema shambulio hilo ni baya na la kijinga, ni moja ya mashambulizi ya kutisha zaidi katika historia ya karibuni ya Kanada. Waziri Mkuu Trudeau ameonyesha huruma zake kwa wale wanaohusika na mkasa uliotokea. Amesema raia wote wanapaswa kujisikia wako salama kutembea katika miji na miongoni mwa jamii. Bwana Trudeau amesema hali hii inafuatiliwa kwa ukaribu, na kwamba Canada itaendelea kufanya kazi na vyombo vya usalama nchini kote kuhakikisha usalama wa wananchi wake. Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau Waziri wa usalama wa umma nchini Canada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili  tahadhari katika kiwango cha mashambulizi ya kigaidi. Waziri wa usalama wa umma nchini Kanada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili tah...