Marubani wanafunzi wa Afrika Kusini, waliotengeneza ndege aina ya Sling 4, wamewasili Kilimanjaro,Tanzania, wakiwa njiani kuelekea kwenye kituo chao cha mwisho, jijini Cairo. Timu ya wanafunzi hao waliondoka Zanzibar siku ya Jumapili, baada ya kutumia siku kadhaa bila mafanikio kuzungumza na mamlaka za nchini Kenya ili waweze kutua jijini Nairobi. ''Mamlaka nchini Kenya wamesema hawajafurahishwa na njia zetu hivyo wakatuzuia kuingia,'' alisema kiongozi wa wanafunzi hao, Des Werner, Baba wa Megan Werner 17, mwanzilishi waU-Dream Global. ''Tunaweza kubadili njia lakini hatuna muda wa kufanya hivyo.Tunafikiri kama ni wagumu tusilazimishe kwenda. Hata hivyo ni nchi yao ndio inayokosa nafasi ya vijana wa nchini kwao kuzungumza na timu yetu kwa ajili ya kuwapa msukumo vijana wa nchini mwao.'' Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi yatua Zanzibar Wanafunzi kuendesha ndege kutoka Afrika Kusini mpaka Misri Marubani hao wataelekea Uganda siku ya Jumanne l...