Aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W. Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94 huko mjini Houston, msemaji wake Jim McGrath amethibitisha kifo chake. George H.W. Bush Rais huyo wa zamani wa Marekani aliongoza kwa awamu moja tu akiingia madarakani mwaka 1989 na kuondoka 1993 hivyo kubaki kama Rais pekee aliyeiongoza Marekani kwa awamu moja. Chanzo cha kifo cha George Bush hakijawekwa wazi rasmi, lakini Rais huyo mstaafu wa Marekani, kwa muda mrefu alikuwa akipambana na ugonjwa wa 'Vascular Parkinsonism', na kifo chake kimetokea ikiwa imepita miezi michache tangu mke wake Barbara Bush afariki dunia mnamo April 17, 2018 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Taarifa zaidi zinasema kwamba George Bush alikumbwa na ugonjwa huo tangu miaka ya 90, na mwenyewe aliwahi kuulezea kuwa ni ugonjwa mzuri kuupata kwani haumuumizi, isipokuwa tu anashindwa ku-'move' pale anapotaka hata kunyanyua mguu. "Unaathiri miguu, hauumii, unaiambia miguu yako ijongee na haijon...