Diamond Platnumz na ATCL: Mwanamuziki azozana na Air Tanzania kuhusu kuachwa na ndege uwanjani Mwanza
Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Diamond Platnumz ametofautiana na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuhusu kilichotokea hadi akaachwa na ndege uwanjani mwanza. Mwanamuziki huyo anasema tamko lililotolewa na shirika hilo kwamba alichelewa kufika uwanjani si za kweli. ATCL kupitia taarifa wamesema Diamond , ambaye wamemrejelea kama Isaack Nasibu, alikuwa miongoni mwa abiria waliopaswa kusafiri na ndege ya shirika hilo Jumapili 16 Desemba, 2018 hakuachwa kama inavyodaiwa bali alichelewa kufika uwanjani kwa muda unaotakikana. Anadaiwa kufika dirishani robo saa baada ya dirisha kufungwa. Jina rasmi la mwanamuziki huyo ni Nasibu Abdul Juma Issaack. "Kampuni inapenda kutoa ufafanuzi kuwa abiria huyo alifika uwanjani kwa kuchelewa na hivyo kuzuiliwa na mamlaka zinazosimamia uwanja kwa mujibu na taratibu," ATCL wamesema. Aidha, shirika hilo la serikali limepuuzilia mbali madai ya msanii huyo kwamba tiketi yake iliuzwa kwa abiria wengine. "Kampuni inapenda kutoa ufaf...