Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MWANZA

Bakwata yarejesha kiwanja chake, Waislamu kupiga dua maalum kuishukuru Mahakama

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) mkoa wa Mwanza limerejesha umiliki wa kiwanja namba 111 kitalu T kilichopo Kenyatta Road jijini hapa kwenye eneo maarufu la 'Muslim' (ilipo stendi ya Igombe) kilichokuwa kimechukuliwa na halmashauri ya Jiji la Mwanza.   Bakwata imerejesha umiliki huo baada ya kushinda kesi kufuatia halmashauri ya Jiji la Mwanza kushindwa kutimiza masharti iliyopewa na mahakama.   Shauri hilo namba 150 ya mwaka 2020 lililotokana na kesi namba 58 ya mwaka 2017 liliamuliwa Juni 3, 2022 ambapo Mahakama ilithibitisha kwamba kiwanja hicho ni mali halali ya Bakwata.   Akitoa taarifa kwa umma wa kiislam leo Juni 5, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Bakwata jijini Mwanza, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hasani Kabeke amesema katika uamuzi wake mahakama ilitoa masharti mawili kwa halmashauri ya Jiji ikitakiwa kulipa fidia ili kukitwaa kiwanja hicho ama irudishe kiwanja hicho kama fidia itashindwa kufikiwa ndani ya miezi mitatu, ambapo...

Mtoto wa siku mbili atupwa kandokando ya ziwa Victoria

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limefanikiwa kumuokota mtoto mmoja wa kike akiwa hai anayekadiriwa kuwa na umri wa siku 2 hadi 3 baada ya kutupwa kichakani kandokando mwa ziwa Victoria na mtu asiyefahamika maeneo ya Bwiru ziwani Wilayani Ilemela.  Tukio hilo limetokea Novemba 1, 2018  hii ni baada ya watu waliokua wakipita njiani kusikia sauti ya mtoto akilia toka kichakani ndipo walifuatilia na walipoona ni mtoto walitoa taatifa Polisi.  Polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kukuta mtoto wa kike akiwa ametupwa kichakani hapo akiwa hai huku mwili wake ukiwa umeviringishwa kwenye mfuko wa sandarusi.  Jeshi la Polisi limeeleza kuwa Mtoto huyo amepata matibabu na hali yake inaendelea vizuri amekabidhiwa katika shirika la Forever Angel lililopo Bwiru Wilayani  Ilemela kwa ajili ya hifadhi.  Hata hivyo Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi pamoja na msako mkali wa kumtafuta mama wa mtoto huyo