S imba ya Tanzania na Gor Mahia ya Kenya zapewa wapinzani Droo ya kombe la Vilabu bingwa barani Afrika hatimaye imetolewa. Katika michuano hiyo klabu ya Simba kutoka nchini Tanzania imepangwa kucheza dhidi ya mabingwa wa zamani wa kombe hilo TP Mazembe wa DR Congo huku mabingwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia wakimenyana dhidi ya klabu ya S Berkane kutoka Morocco. Droo hiyo iliofanyika siku ya Jumatano katika mji wa mkuu wa Misri, Cairo iliwakutanisha mabingwa hao huku safari ya michuano hiyo ikielekea kufika ukingoni. Baadhi ya magwiji wa kandanda waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na naibu katibu mkuu wa CAF Anthony Baffoe, chini ya usaidizi wa mshambuliaji wa zamani wa Cameroon Patrick Mboma pamoja na Emad Moteab kutoka Misri. Pia baadhi ya waliohudhuria walikuwa wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki. Jinsi Simba na Gor M ahia zilivyotinga robo fainali Katika hatua ya kuelekea robo fainali klabu ya Simba ya Tanzania ilivunja mwiko wa miaka 25 baada ya kuilaza klabu ya Vit...