Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TAKUKURU

Mwalimu kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa

Mwalimu kuburuzwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa Taassis ya kuzuaia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara inatarajia kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Masasi, Mwanaid Abdalah Mtaka kwa tuhuma za kutumia nyaraka za uongo na kujipatia fedha kiasi cha Shilingi 1,578,000. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Takukuru Mkoani humo, Stephen Mafipa , amesema kuwa Mtaka anakabiliwa na kosa la jinai kwa kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake kisha kujipatia kiasi hicho cha fedha jambo ambalo ni kinyume na sheria. “Alitumia na kuwasilisha stakabadhi zenye kuonyesha alitumia jumla ya shilingi 1,578,000/= kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya shule ya Msingi Masasi, hukub akijua kwamba hakununua,”Amesema Mafipa. Aidha, kitendo hicho kilimuwezesha mtuhumiwa kujipatia kiasi cha shilingi 1,578,000/= ambazo alizitumia kwa matumizi yake binafsi. Kesi hiyo ya Jinai itafunguliwa katika mahakama ya wilaya...

Mama Samia aionya Takukuru kukumbatia wala rushwa

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ameionya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Rombo kutokana na taarifa kwamba baadhi ya maofisa wake wanatumika kuwalinda watendaji wa serikali wanaojihusisha na rushwa.  Samia alitoa onyo hilo jana akiwa katika sehemu ya ziara yake ya siku tano ya kikazi mkoani Kilimanjaro.  Alisema asilimia 90 ya watendaji wa serikali katika wilaya hiyo wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wakutoa huduma kwa wananchi, huku akiionyooshea kidole taasisi hiyo kwa kuwafumbia macho watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rombo.  "Nasikitika kusema kuwa asilimia 90 ya watendaji wa halmashauri wanafanya kazi kwa kupokea rushwa ili kuwaudumia wananchi. Niwaonye na niwaambie taarifa hizo tunazo na majina yenu tunayo. Jirekebisheni mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.  “Takukuru sidhani kama mnatambua wajibu wenu au nimeona jengo tu ambalo halina utendaji? Wananchi wengi wanashindwa kup...