MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Baadhi ya waliohudhuria tamasha hilo wakitoroka kufuatia shambulio la bwana Paddock Rais Donald Trump wa Marekani amemtaja muuaji wa watu 59 huku 527 wakijeruhiwa mjini Las Vegas kuwa mgonjwa aliye na akili punguani. Akizungumza katika ikulu ya Whitehouse , amesema kuwa ataziangazia upya sheria za umiliki wa bunduki katika siku za usoni lakini hakuelezea zaidi. Maafisa wa polisi wanajaribu kubaini kwa nini Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa katika tamasha akiwa katika ghorofa ya 32 karibu na hoteli ya Mandalay Bay. Polisi walipata bunduki 23 katika chumba chake pamoja na vilipuzi. Kufikia sasa hakuna sababu mwafaka iliotolewa na wachunguzi hawajapata ishara zozote za shambulio hilo kuhusishwa na ugaidi wa kimataifa. Mshambuliaji aua watu 58 Las Vegas Marekani Polisi watafuta sababu ya mauaji Las Vegas Mauaji Las Vegas: Tunayoyafahamu kufikia sasa Kwa Picha: Mauaji Las Veg...