Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya RAIS

Rais Samia amefungua Mkutano wa 14 wa Baraza la Biashara (TNBC)

  Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo June 09,2023 amefungua na kushiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Biashara (TNBC), Ikulu Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba kazi kubwa inaendelea kufanyika ya kuboresha mifumo ya TEHAMA kwenye Sekta za Umma ili ianze kusomana ambapo ameahidi kuwa sio zaidi ya miezi sita RAISkinachotokea Bandarini atakuwa anaweza kukisoma akiwa Ikulu. Rais za Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Juni, 2023. Rais Samia amenukuliwa akisema “Kazi kubwa inaendelea kufanyika ya kuboresha mifumo ya TEHAMA, mifumo yetu haisomani, taarifa hazioani, kazi tunayokwenda kufanya kwa nguvu kubwa sasa ni kufanya mifumo ndani ya Sekta ya Umma isomane pia iwe na vigezo vya Kimataifa” “Changamoto zilizotajwa hapa hizo za Kariakoo na nini ni kwamba mifumo yetu haijaweza kuchukua taarifa zote hizo, kazi iliyopo sasa ni...

RAIS AWAPA YANGA NDEGE MAALMU KUWAPELEKA MBEYA

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa ndege itakayowapeleka Yanga jijini Mbeya kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.   Awali Yanga walitakiwa kuondoka saa leo saa moja jioni lakini kutokana na mwaliko maalum wa chakula cha jioni Ikulu, Rais amekubali kuwagharamia safari ambapo sasa watasafiri leo saa 5 usiku.   Yanga wamebakisha mechi mbili za kumaliza msimu, ambapo watacheza na Tanzania Prisons na Mbeya City jijini Mbeya.     mteulethebest

Trump aonya juu ya "Kifo na Uharibifu"

 Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ameonya kwamba kunaweza kuwa na "kifo na uharibifu" ikiwa atashtakiwa kwa madai ya kuamuru wakili wake kulipa pesa za kimya kwa nyota wa ponografia Stormy Daniels wakati wa hatua za mwisho za kampeni yake ya urais 2016.  "Ni mtu wa aina gani anaweza kumshtaki mtu mwingine, katika kesi hii Rais wa zamani wa Merika ... na Uhalifu, wakati inajulikana kwa wote kwamba HAKUNA Uhalifu uliotendwa," Trump aliandika katika chapisho la Ukweli wa Jamii mnamo Ijumaa akimaanisha.  kwa Wakili wa Wilaya ya Manhattan Alvin Bragg.  Ingawa hakumtaja kwa jina, Trump anadai mtu huyu, ambaye anamwita "mgonjwa mbaya wa akili ambaye anachukia sana USA," anajua kwamba "kifo na uharibifu unaowezekana katika shtaka kama hilo la uwongo unaweza kuwa janga kwa Nchi yetu."

RAIS WA TANZANIA ATOA TAHADHARI KUJIKINGA NA UGONJWA WA CORANA

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa tahadhari kuhusu ugonjwa unaotokana na virusi vya corona, akiwataka kutopuuza kwani mpaka sasa umegharimu maisha ya watu wengi duniani. Amezungumza na Umma wa Tanzania alipokuwa akizindua karakana ya jeshi hii leo jijini Dar Es Salaam. Katika kusisitiza tahadhari iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa afya nchini humo, Ummy Mwalimu, Rais Magufuli amewataka raia kutopuuza tahadhari hizo. ''Ugonjwa upo na umekumba nchi nyingi kwa takwimu zilizopo ni kwamba zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa na watu 4,500 wamepoteza maisha.'' ''Tunatambua kuwa Tanzania mpaka sasa hatuna mgonjwa wa corona lakini hatuwezi kujiweka pembeni bila kuchukua hatua na hatua zimeanza kuchukuliwa waziri wa wizara ya afya ameshatoa tahadhari tunazopaswa kuchukua''. ''Ugonjwa huu unaua na unaua kwa haraka, sana niwaombe tusipuuze, tusipuuze hata kidogo ni lazima kuchukua hatua za kujikinga...

Victiore Ingabire na Kizito Mihigo waachiliwa huru na rais Paul Kagame Rwanda

Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake kuwaachilia zaidi ya wafungwa 2000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu. Miongoni mwa wafungwa hao waliofaidika na hatua ya rais huyo ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Victoire Ingabire ambaye alikuwa katika kizuizi tangu 2010. Victoire Ingabire alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 kwa kutishia usalama wa serikali na kudunisha mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Amekuwa akiongoza ukosoaji wa rais Paul Kagame huku akiongezea kuwa hukumu yake ilishinikizwa kisiasa. Bwana Kagame amepongezwa kwa kurekebisha uchumi wa Rwanda lakini pia ameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za kibinaadamu. Kuwachiliwa huru kwa bi Ingabire na wafungwa wengine 2,140 kulitangazwa na seriikali kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri. Taarifa ilisema kuwa bwana Kagame aliwaonea huruma chini ya uwezo wake kama rais. Mbali na Ingabire ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alifungwa kwa miaka 10...