Uhuru Kenyatta ameahidi kukabiliana na ufisadi wakati alipochaguliwa kwa mara ya kwanza 2013 Maafisa wakuu wa serikali ya Kenya watalazimika kupimwa kwa kutumia kifaa cha kuwafichua watu waongo ikiwa ni miongoni mwa harakati za kukabiliana na ufisadi , rais Uhuru Kenyatta amesema. Bwana Kenyatta alisema kuwa kifaa hicho ambacho kitafichua maadili ya wafanyikazi ni miongoni mwa mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo. Alikuwa akizungumza baada ya kufichuliwa kwamba shilingi dola bilioni 8 za Kenya zilipotea katika kitengo kimoja cha serikali. Takriban wafanyikazi 40 wa umma wanakabiliwa na mashtaka kufuatia kashfa hiyo. Kashfa hiyo ya ufisadi , ambayo ilifichuliwa na wauzaji bidhaa ambao walikuwa hawajalipwa , ilipelekea kuibiwa kwa fedha hizo katika shirika la vijana wa huduma kwa jamii NYS kupitia vyeti bandia na malipo ya ziada. Uchunguzi huo wa NYS -ukiwa mpango muhimu wa serikali ya rais Kenyatta kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana umeonekana ...