Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Rwanda yapitisha sheria mpya kupambana na uhalifu wa mtandaoni


Bado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi.

Bunge nchini Rwanda, Alhamisi lilipitisha sheria ya uhalifu wa mtandaoni yenye nia ya kuisaidia sekta za kiserikali na binafsi kudhibiti uhalifu huo.


Bunge la juu lilipitisha muswada na kupeleka kwenye bunge dogo. Bado muswada unahitaji kupitishwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame kabla ya kuanza kufanya kazi.


Sheria inalenga kulinda taarifa za serikali na binafsi na miundombinu dhidi ya uhalifu wa mitandaoni na mashambulizi ya mitandaoni, kwa mujibu wa Wizara ya habari na mawasiliano na Teknolojia ya Rwanda.


''kwa sasa tunashuhudia mashambulizi ya mitandaoni duniani kote. Mashambulizi ambayo yanatishia usalama wa uchumi na usalama wa taifa,'' alieleza Agnes Mukazibera, Rais wa Bunge la Rwanda, baada ya kura.


Sheria itaisaidia serikali kufanya uchunguzi vitisho vyovyote na kushtaki dhidi ya vitendo hivyo katika taasisi binafsi na za umma na kuitetea nchi dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni.


Je ni kweli sheria mpya ya Uhalifu wa Mtandao itakandamiza uhuru wa kujieleza Kenya ?

Mwaka 2016 Rwanda ilidhibiti zaidi ya mashambulizi ya mitandaoni 1,000 kila siku kabla ya kuleta madhara kwa walengwa,makampuni na taasisi,kwa mujibu wa Benki kuu Rwanda.


Mwaka huo huo, Rwanda ilizindua mfumo wa usalama wa mtandao uliogharimu dola za kimarekani milioni tatu kwa ajili ya kulinda taasisi binafsi na za serikali dhidi ya uhalifu wa mitandaoni.


Kwa mujibu wa utafiti, Kenya ni nchi inayoshambuliwa zaidi na wahalifu wa mitandaoni katika eneo la Afrika Mashariki, huku biashara nchini humo zikipoteza kiasi cha dola milioni 146 kutokana na uhalifu wa mitandaoni.


Kampeni ya kuwasaka wanaoeneza habari za uongo Afrika mashariki


Rwanda inakuwa nchi nyingine katika Afrika mashariki kuidhinisha sheria zinazolenga uhalifu katika mitandao.


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliidhinisha mswada wa Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni wa 2018 kuwa Sheria, hatua itakayotoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makosa ya mtandaoni.


Sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya Sh5 milioni (dola 50,000 za Marekani) au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi.



PSCU

Sheria mpya Kenya ya kupambana na uhalifu katika mtandao inafuata nyingine kama hiyo katika mataifa ya Afrika Mashariki kuwaadhibu watu wanaosambaza 'habari za uongo'na kutoa adhabu kali kwa wahalifu wa mitandaoni.


Hali sio tofuati sana katika nchi jirani ya Tanzania ambapo maafisa hivi maajuzi walitangaza sheria mpya zinazowahitaji wanablogu kulipa .


Serikali inasema inataka kulilinda taifa hilo dhidi ya 'uongo' unaosambazwa katika mitandao, licha ya kwamba wakosoaji wanaiona hatua hiyo kama njia ya kukandamiza uhuru wa kujieleza.


Rais John Magufuli amesema ananuia kukabiliana na anachokitaja kuwa ni 'ugonjwa'.



Rais John Magufuli ameunga mkono sheria hiyo Tanzania

Hatahivyo mahakama kuu nchini ilizuia utekelezaji wa sheria hiyo mnamo Mei 5 baada ya kundi la wanaharakati na wawakilishi kutoka vyombo vya habari nchini kuzusha pingamizi.


Iwapo sheria hiyo itapita kesi iliyopo kotini, inatoa adhabu ya faini isiyo chini ya $2,000 au kifungo kisicho chini ya mwaka mmoja au yote mawili kwa wahalifu watakaopatikana na makosa.



Nchini Uganda, serikali ya rais Yoweri Museveni imezuia mipango ya kuidhinisha kodi ya kutumia mitandao ya kijamii baada ya wizara ya fedha kusema inahitaji kushauriana kuhusu vipi mpango huo wa kodi utaweza kuidhinishwa.



Rais Museveni alipendekeza kuidhinisha kodi ya kutumia mitandao ya kijamii

Museveni alipendekeza watu watozwe kodi kwa kutumia mitandao ya kijamii Facebook na WhatsApp, akisema kodi itakayokusanywa italisaidia taifa hilo kukabiliana na athari za Olugambo [uvumi]".


Wakosaji wanasema nia ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 73 ni kukandamiza vyombo vya habari na wale wanaopinga mpango wake wa kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu wa 2021.


Serikali yake ilifunga mitandao ya kijamii wakati wa uchaguzi mkuu mnamo 2016


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...