Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MKATABA

TRUMP AVUNZA MKATABA KUMKERA BARACK OBAMA SIRI HADHARANI

Barua mpya iliyovuja yadai Trump amevunja mkataba wa nyukilia 'ili kumkera Obama' Rais Donald Trump ameachana na mkataba wa nyukilia wa Iran ili kumkera Barack Obama, hiyo ni kwa mujibu wa barua ya siri iliyovuja kutoka kwa aliyekuwa balozi wa Uingereza nchini Marekani. Sir Kim Darroch alielezea hatua ya Trump kuvunja mkataba huo kama "ubadhirifu wa kidiplomasia" kwa mujibu wa gazeti la Mail on Sunday. Gazeti hilo linadai kuwa barua hiyo iliandikwa baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Borris Johnson kuirai Marekani mwaka 2018 kusalia ndani ya makubaliano hayo. Barua hii mpya inavuja katikakipindi ambacho polisis nchini Uingereza wameonya juu ya uchapishwaji wa barua hizo. Barua ya kwanza kutoka kwa balozi huyo ambayo ilikuwa inakosoa utawala wa Trump ilivuja wiki moja iliyopita na kusababisha majibizano ya hasira baina ya Uingereza na Marekani. Majibizano hayo yamesababisha Sir Kim kujiengua kwenye wadhifa wake licha ya serikali ya ...