Uturuki imepokea shehena ya kwanza ya makombora ya Kirusi ya S-400 licha ya upinzani mkali kutoka Marekani
Makombora ya Kirusi yawasili Uturuki licha ya vikwazo vya Marekani Makombora ya S-400 ni moja ya zana hatari zaidi za kutungua ndege angani Uturuki imepokea shehena ya kwanza ya makombora ya Kirusi ya S-400 licha ya upinzani mkali kutoka Marekani . Shehena hiyo imepokelewa katika uwanja wa ndege wa jeshi leo Ijumaa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara. Hatua hiyo ya Uturuki kwa hakika itaikasirisha Marekani ambayo tarayi imeshaonya kuwa nchi hiyo haiwezi kumiliki zana za kijeshi za Urusi na Marekani kwa pamoja. Makombora ya S-400 kutoka Urusi ni ya kujilinda na ndege vita, na wakati hu huo Uturuki imewekeza vilivyo katika ununuzi wa ndege vita aina ya F-35 kutoka Marekani. Mzozo unatoka wapi ? Uturuki imeshasaini mkataba wa kununua ndege vita 100 aina ya F-35 kutoka Marekani. Pia kampuni za Kituruki zinatengeneza takribani vipuri 937 vya aina hiyo ya ndege. Uturuki na Marekani zote ni nchi wananchama wa Umoja wa Kujihami wa Nato, ambapo Urusi yaonekana ni adui mkuu ...