Mwanadada Elizabeth Michael amemaliza rasmi kifungo chake alichokuwa akitumikia kwa muda saa akiwa nje na November 12 ndio ilitakiwa kuwa huru kwa kukimaliza kifungo hicho. Mwanadada Lulu ambae alikuwa nje akitumia kifungo cha nje huku akipangi wa kufanya kazi mbalimbali za kijamii amekuwa huru kuanzia sasa na kwamba hata zile kazi alizokuwa akifanya za kijamii itakuwa zimefika kikomoe kuanzia sasa. Lulu alihukumiwa kifungo cha jela baada ya kukitwa na kesi ya kuua bila kukusudia kwa mwanamaigizo mwenzake Steven Kanumba mabae alikuwa ni mpenzi wake pia walipokuwa wakikorofisha na kumsukuma kwa bahati mbaya na kuuumia sehemu za kichwa. Mwanadada Lulu anaingia uraia tena akiwa tayari amevishwa pete ya uchumba na mpenzi wake wa siku nyingi Majizo ambao walitangaza ndoa hiv karibuni