Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SYRIA

Marekani Yafanya Mashambulio ya Anga ya Kulipiza kisasi nchini Syria

 Jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi ya anga yaliyosahihi nchini Syria kujibu shambulio la ndege isiyo na rubani na kumuua mwanakandarasi mmoja wa Marekani na kuwajeruhi wafanyakazi watano wa Marekani.  Shambulio la awali lilifanywa na, na mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya, "makundi yenye uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran", kulingana na Idara ya Ulinzi.  "Mashambulizi hayo ya anga yalifanywa kujibu mashambulizi ya leo pamoja na mfululizo wa mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya vikosi vya Muungano nchini Syria na makundi yenye uhusiano na IRGC," Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin alisema.  Jiandikishe kwa RT

Rais wa Syria Bashar al- Assad kutembelea Korea Kaskazini

Kauli ya Assad imeripotiwa kutolewa a;ipokutana na Balozi mpya wa Korea Kaskazini nchini Syria Rais wa Syria, Bashar al-Assad anapanga kutembelea nchini Korea Kaskazini,Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeeleza. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuhodhi ziara ya Kiongozi wa nchi tangu alipoingia marakani mwaka 2011 Hivi karibuni amekuwa na shughuli nyingi za kidiplomasia, kukutana na Rais wa China mwezi Mei na anatarajiwa kuhudhuria mkutano na Donald Trump mwezi huu Syria, mshirika wa Korea Kaskazini, haijasema lolote kuhusu mpango huo unaoripotiwa. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishutumiwa kushirikiana katika mapngo wa kutumia silaha za kemikali.Lakini nchi hizi zimekana shutuma hizo Tarehe ya ziara hiyo haijawekwa wazina vyombo vya Korea Kaskazini. Vilimnukuu bwana Assad siku ya Jumatano akisema ''ninakwenda kutembelea Korea Kaskazini na kukutana na Kim Jong-un." Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi...

Yanayoendelea nchini Syria

Jeshi la Syria leo limelishambulia kwa mabomu eneo mojawapo la waasi huku makubaliano ya kuwaondoa waasi hao yakiwa yamefikiwa na rais Assad anaendeleza mkakati wa kuikomboa ngome ya mwisho ya waasi. Vyombo vya habari vya serikali vya nchini Syria vimearifu juu yakufikiwa makubaliano juu ya kuwahamisha wapiganaji wanaohusishwa na kundi la al-Qaida kutoka kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina iliyopo karibu na mji wa Damascus, na kisha badala yake kuachiwa huru watu kadhaa waliokuwa wanashikiliwa na waasi kwa miaka mingi. Mgogoro wa Syria Mapema leo jeshi la Syria liliushambulia kutoka angani mji wa Rastan na vijiji vilivyo karibu na miji ya waasi ya Hama na Homs. Kwa mujibu wa Shirika linalo tetea Haki za Binadamu nchini Syria majeshi ya serikali yamefanya mashambulizi ya anga zaidi ya 140. Waasi wa Syria wanashikilia maeneo makubwa huko kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Syria. Muungano wa wanamgambo wa Kikurdi na ule wa Kiarabu unaoungwa mkono na Marekani u...

Mashambulizi dhidi ya Syria hayakuwa halali-Ripoti ya Bunge la Ujerumani

Ripoti ya wataalamu wa masuala ya sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani imesema mashambulizi yaliyofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Syria mapema mwezi Aprili yalikiuka sheria ya kimataifa. Ripoti ya wataalamu wa sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani, imesema mashambulizi yaliyofanywa na nchi tatu za Magharibi hayakuwa halali kisheria. Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliishambulia Syria kwa makombora tarehe 14 Aprili, kwa madai kwamba zilikuwa zikiiadhibu serikali ya Rais Bashar al-Assad, ziliyemshutumu kutumia gesi ya sumu kuwashambulia raia katika mji wa Douma. ''Matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya nchi huru, kama hatua dhidi ya ukiukaji wa sheria na kanuni za kimataifa unaodaiwa kufanywa na nchi inayoshambuliwa, ni uvunjaji a sheria ya kimataifa inayozuia matumizi ya ghasia,'' imesema ripoti hiyo ya wataalamu wa kisheria wa Bunge la Ujerumani, Bundestag. Ripoti hiyo iliombwa na chama cha mrengo wa kushoto (Die-Linke) cha Uj...

Bashar al-Assad arudisha tuzo aliyopewa na Ufaransa

Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia balozi ya Roma mjini Damascus. Syria imerejesha kwa Ufaransa tuzo ya Légion d'honneur aliyopewa rais Bashar al-Assad, ikisema kuwa haiwezi kuchukua tuzo kwa taifa ambalo limekuwa 'mtumwa' wa Marekani. Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya Ufaransa kusema kuwa adhabu ya kuikataa tuzo hiyo inakaribia. Ufaransa hivi majuzi ilijiunga na Ufaransa na Uingreza katika kuishambulia Syria kufuatia madai ya kutumia silaha za kinyuklia dhidi ya raia wake. Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia balozi ya Roma mjini Damascus. Rais Assad alipewa tuzo hiyo ya hadhi ya juu 2001 baada ya kuchukua mamlaka kufautia kifo cha babake. ''Wizara ya maswala ya kigeni imerudisha kwa Jamhuri ya Ufaransa tuzo ya Légion d'honneuri iliopewa rais Assad'', wizara ya kigeni nchini Syria ilisema katika taarifa. ''Sio heshima kwa rais Assad kuvaa tuzo iliotolewa na taifa la utumwa na mshiriki wa taifa la Marekani li...

Shambulio la kemikali nchini Syria: Wachunguzi waruhusiwa kuzuru Douma

Wakaazi wakitembea karibu na eneo lililodaiwa kushambuliwa na kemikali Douma siku ya Jumapili wiki moja baada ya shambulio Wachunguzi wa silaha za kemikali nchini Syria wataruhusiwa kuzuru katika eneo linalodaiwa kushambuliwa na silaha za sumu siku ya Jumatano, kulingana na uUrusi. Kundi hilo la kimataifa limekuwa nchini humo tangu siku ya Jumamosi lakini halijaruhusiwa kuingia Douma. Shambulio hilo la siku ya Aprili 7 lilivutia shambulio dhidi ya serikali ya Syria lililotekelezwa kwa pamoja na Marekani, Uingereza na Ufaransa wiki moja baadaye. Syria na mshirika wake Urusi wamekana shambulio lolote la kemikali huku Urusi ikitaja madai hayo kama 'yaliopangwa'. Mapema siku ya Jumanne , chombo cha habari cha Syria kilisema kuwa ulinzi wa angani wa taifa hilo ulikabiliana na shambulio la makombora juu ya nga ya magharibi mwa mji wa Homs. Makombora hayo yalilenga kambi za wanahewa wa Shayrat lakini haikusema ni nani aliyetekeleza mashambulio hayo. Image cap...