Msanii wa kike wa Hip Hop kwenye muziki wa Bongo Fleva, Chemical, ametangaza kutafuta mwanaume ambaye atakuwa mkweli ili awe naye kwenye mahusiano kwa malengo ya kufunga naye ndoa. Chemical amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba iwapo atatokea mwanaume ambaye atakuwa 'serious', hatosita kuwa naye. Kabla ya kufikia uamuzi huo Chemical alielezea juu ya kitendo cha kumtosa Stereo, na kusema kwamba msanii huyo alikuwa anamjaribu lakini aligundua hakuwa mkweli kwake, ndio maana ameamua kutafuta mtu ambaye atakuwa 'serious' naye. 'Wanaume wengi wanaumiza, kuna watu wanahisi Chemical haingii kwenye mahusiano, mimi ni mdada jamani naingia kwenye mahusiano, moyo wangu uko very delicate hivyo sipendi kuumizwa moyo, lakini akitokea mwanaume wa ukweli ambaye hatamuumiza Chemical, niko tayari kupenda na kupendwa, Stereo alikuwa anataka kunichezea, sijui alikuwa anataka kujaribu, hakuwa serious, mimi nilijifanya kumkataa kidogo tu akapat...