mteulethebest
Rais wa Tanzani, John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara (VPL) kati ya mabingwa wapya Simba SC na Kagera Sugar utakaochezwa Jumamosi Mei 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema wamemuandikia barua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kumuomba Rais Magufuli awe mgeni Rasmi kwenye mchezo huo.
Karia ameeleza kuwa Rais Magufuli endapo atakubali wito huo, atapata nafasi ya kuwakabidhi Simba Kombe la VPL, sanjari na kuikabidhi Timu ya Taifa ya soka ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kombe la CECAFA kwa vijana walilotwaa siku za karibuni nchini Burundi.
Amesema mchezo kati ya Simba na Kagera Sugar utaanza saa 8:00 mchana badala ya Jumapili saa 10:00 jioni ili kutoa fursa kwa sherehe hizo kufanyika kikamilifu.
Maoni