Mkusanyiko wa picha za kuvutia zaidi kutoka kwa harusi ya kifalme kati ya MwanamfalmeHarry na Meghan Markle.
Umati ulishangilia Mwanamfalme Harry, ambaye sasa atakuwa Mtawala wa Sussex, na mkewe Meghan, Mke wa Mtawala wa Sussex, walipopitia kwenye barabara za mji wakiwa kwenye kigari cha kuvutwa kwa farasi
Inakadiriwa kwamba 100,000 walijitokeza barabara za Windsor
Umati wa watu ulikusanyika kando ya barabara kutazama msafara wa harusi ukipita
Meghan na Mwanamfalme Harry wakiondoka kanisa la St George
Ragland, mamake bi harusi, Charles Mtawala wa Cornwall (babake Harry) na mkewe Camilla wakiondoka kanisani Wakiondoka kanisani
Waliokuwemo walishangilia wawili hao walipokuwa wanapigana busu
Wawili hao wakipigana busu
Wawili hao wakiondoka kanisani baada ya kufunganishwa katika ndoa
Harry na Meghan sasa watakuwa Mtawala na Mke wa Mtawala wa Sussex
Malkia na mumewe, Mwanamfalme Phillip walihudhuria sherehe hiyo
Mwanamfalme Harry akimfunua Meghan
Kasisi Michael Curry, mkuu wa kanisa la Episcopal la Marekani ndiye aliyetoa mahubiri, ambapo aliangazia dhana ya upendo
Mwanamfalme Harry na Meghan Markle
Bi Markle alipokelewa na Mwanamfalme Charles (babake Harry) na kusindikizwa hadi kwenye madhabahu. babake, Thomas, anaugua
Bi Markle na wasichana na wavulana wasaidizi wa harusi wakiingia kanisani. Mwanamfalme George na Bintimfalme Charlotte walikuwa miongoni mwa wasimamizi wa harusi hiyoMeghan Markle alifika Windsor Castle akiwa amevalia vazi la harusi lililokuwa limeshonwa na Mwingereza Claire Waight Keller
Meghan Markle aliondoka hotelini alimolala kuelekea Windsor Castle akiwa na mamake Doria
Mke wa Mwanamfalme William, Kate, aliwasili na wasichana na wavulana waliosimamia harusi hiyo
Mwanamfalme Harry alionekana mtulivu akiwapungia mkono waliokuwa wamefia kufuatilia harusi hiyo, alipokuwa anaelekea kanisani na kakake
Mwanamfalme Harry na Meghan Markle katika kanisa la St George kasri la Windsor Castle
Image captionBi Meghan Markle akiwasili Windsor Castle
Mwanamfalme Harry na msimamizi wake kwenye harusi, kakake Mwanamfalme William
Bi Markle akiondoka hoteli ya Cliveden House akiandamana na mamake Doria
Watu wengi wamekusanyika Windsor kufuatilia harusi hiyo
Watu hadi 100,000 wanatarajiwa kukaa kwenye barabara za mji huo kutazama msafara wa harusi
Wengi walifika kwa treni, magari na mabasi kutoka kila pembe na Uingereza na hata nje ya nchi hiyo
Waliofika wakitembea kwenye barabara inayofahamika kama Long Walk kuelekea Windsor Castle.
Baadhi walikesha karibu na Windsor usiku kuhakikisha wanapata nafasi bora zaidi ya kujionea msafara wa harusi
Wageni mashuhuri, wakiwemo Oprah Winfrey na Idris Elba, wamefika kwa sherehe hiyo St George's Chapel, Windsor Castle
Watu wa kawaida 1,200 - wengi wao wafanya kazi wa kusaidia jamii - walialikwa kwa harusi hiyoKanisa la St George limepambwa kwa maua na matawi
Kanisa la St George ndani ambapo pia limepambwa kwa maua na matawi
Maoni