Watu zaidi ya 10 wamefariki kutokana na uhaba wa chakula Turkana County Zaidi ya watu 800,000 wanaendelea kuumia kwa makali ya njaa na kiu kwa mujibu wa wizara ya kudhibiti majanga na utumishi wa umma ya kaunti ya Turkana. BBC Huyu ni mama Audan Loteng' Takwa aliye na umri wa miaka 63. Anaelezea masaibu anayopitia yeye na wanakijiji wenzake ambao wanahofia huenda wakaangamia kwa njaa iki serikali ya Kenya haitaingilia kati hali yao. BBC Anna Emaret anasema amekuwa akigawana chakula na mifugo wake, lakini chakula kilipoisha, wakafa. BBC Mama huyu ana ujauzito wa miezi sita na hajakula chochoto kwa siku tatu zilizopita. BBC Mariam Loolio ni ajuza mwenye umri was miaka 85. Kwa siku tano anasema hajala chochote. BBC Kwa mujibu wa mtazamo kuhusu uwepo wa chakula cha kutosha kwa Kenya 2019 , baadhi ya maeneo ya mashariki, kaskazini na kaskazini magharibi mwa Kenya ambapo kuna jamii za wafugaji, huenda zikakabiliwa na mzozo wa uhaba wa chakula. ...