RAIS wa Urusi, Vladimir Putin. RAIS wa Urusi, Vladimir Putin akiwa amebakiza siku chache kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu, ameanika kiasi cha fedha alizojipatia kipindi cha miaka mitano iliyopita ambacho si kikubwa kama ambavyo ilifikiriwa. Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Shirikisho la Urusi imeeleza kuwa, Rais Putin alijipatia mapato ya Rouble Milioni 38.5 za Urusi sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 1.9 kati ya mwaka 2011 na 2016. Hiyo maana yake ni kwamba kiongozi huyo wa nchi ya Urusi ana mshahara wa Dola za Kimarekani 143,000 kwa mwaka. Fedha hizo hazizidi hata theluthi moja ya ule anaopokea Waziri Mkuu wa Australia, Malcom Turnbull ambaye hulipwa Dola za Kimarekani 527,852. Kwa mujibu wa Gazeti la Washington Post, Rais Putin pia ameorodhesha akaunti 13 za benki mbalimbali ambazo kwa pamoja zina akiba ya Dola za Kimarekani 307,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 650. Rais Putin pia ameorodhesha kumiliki nyumba zake mjini St Petersburg, ...