MTEULE THE BEST Tetemeko laporomosha majumba Italia Image copyright @MONKSOFNORCIA Image caption Inasemekana kuwa watawa walinusurika kwa kukimbia kutoka ndani ya kanisa hili la mtakatifu Benedict mjini Norcia lililoporomoka Tetemeko lingine baya la ardhi, limegonga maeneo ya katikati mwa Italia, mahali ambapo watu 300 waliuwawa mwezi Agosti mwaka huu. Idara ya Seisomologia nchini Italia inakadiria kuwa tetemeko hilo lilikuwa lenye nguvu ya 6.5 katika vipimo vya Richa, tetemeko baya zaidi tangu lilile lililoitetemesha Italia mwaka 1980, iliyowauwa watu elfu 2,400. Image copyright SABRINA FATAUZZI Image caption Majumba yaliyonusurika tetemeko la Julya sasa yameporomoka Tetemeko la sasa limeporomosha jengo la kale la kanisa la mtakatifu Benedict mjini Norcia, pale wamonaki na watawa walikuwa wamekusanyika. Meya wa mji ulioko karibu wa Ussita- Marco Rinaldi, amesema kuwa alikodolea macho kuzimu, kwani kila kitu kilichomzunguka kiliporomoka akitazama. Image copyright @FRAN...