Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba 3, 2017

Rais Magufuli awasamehe wafungwa 61 wa kunyongwa    

Rais Dkt John Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa wa kunyongwa na wale maisha. Rais wa Tanzania John Magufuli kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo amewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Hata hivyo idadi ya wafungwa wengine walioachiwa huru kutokana na makossa mbali mbali ni 1,821 ambao amesema kuwa wanapaswa kuachiwa mara baada ya tangazo lake. Wafungwa wengine 8157 wamepunguziwa adhabu zao. Idadi hiyo ya msamaha kwa wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha wafungwa wa kunyongwa na vifungo vya maisha

Wilshere na Walcott wanataka Wenger ajikune kichwa

Jack Wilshere Jack Wilshere na Theo Walcott wanatumai kwamba meneja wa Arsenal Arsene Wenger atafurahishwa kiasi cha kuwatumia kwenye mechi baada yao kucheza vyema sana Alhamisi. Walciheza vizuri sana mechi ya Europa League ambayo walishinda kwa mabao mengi dhidi ya Bate Borisov. Wawili hao hawajapewa nafasi ya kucheza kikosi cha kuanza mechi Arsenal katika Ligi ya Premia msimu huu, lakini wote wawili walitikisa wavu na kusaidia Arsenal kulaza Bate Borisov 6-0 na kumaliza mechi za Kundi H kwa ushindi. "Kuna ushindani mkali unapokuwa unachezea Arsenal. Tufanya kadiri ya uwezo wetu kumfanya meneja ajikune kichwa akijaribu kuchagua wachezaji wa kutumia," Walcott amesema. Wilshere, aliyefunga bao lake la kwanza tangu Mei 2015 aliongeza, "Jambo tunaloweza kufanya tunapopewa fursa na kumfanya meneja ajikune kichwa." Arsenal walijiweka kifua mbele kupitia Mathieu Debuchy, kisha Walcott akafunga akifuatiwa na Wilshere. Jack Wilshere amechezesh...

Papa Francis anataka maombi ya Baba Yetu yarekebishwe

MTEULE THE BEST Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba maombi maarufu ya Kikristo ya Baba Yetu yafanyiwe marekebisho. Anataka sehemu ambayo huzungumzia vishawishi ilitafsiriwa vibaya. Asema tafsiri kwamba "Usitutie katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" iangaziwe upya akisema tafsiri iliyofanywa si sahihi kwa sababu Mungu huwa hawaongozi binadamu kutenda dhambi. Papa amependekeza watu watumie "usituache tukaingia katika vishawishi (majaribu/majaribuni)" badala yake. Alitoa pendekezo hilo akizungumza katika runinga ya Italia Jumatano usiku. Ombi la Baba Yetu ndilo linalofahamika vyema zaidi miongoni mwa maombi ya Kikristo. Papa Francis amesema Kanisa Katoliki nchini Ufaransa sasa linatumia tafsiri hiyo ya "usituache tukaingia katika vishawishi" kama mbadala, na kwamba jambo kama hilo linafaa kufanywa kote duniani. "Usiniache nikaingia kwenye vishawishi kwa sababu ni mimi nitakayeanguka, si Mungu anayetutia kati...

TANZIA: Walinda amani wa Tanzania wauawa DR Congo

MTEULE THE BEST Umoja wa Mataifa umethibitisha kwamba walinda amani 14 wa muungano huo waliuawa na wengine 53 kujeruhiwa baada ya kambi yao kuvamiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kati ya waliouawa, angalau wanajeshi 12 walitoka Tanzania. Katibu mkuu huyo ameshutumu vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu wa kivita. Ameitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika wanafaa kuwajibishwa. Wanajeshi zaidi wametumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi. Bw Guterres amesema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni. "Ningependa kueleza kusikitishwa kwangu na shambulio hilo lililotekelezwa usiku wa jana dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC. "Taarifa za mwanzo mwanzo eneo la shambulio eneo la Kivu...

Jerry Murro thamani yangu ni zaidi ya wabunge 10 wachadema

MTEULE THE BEST Jerry Murro: Mimi ni sawa na wabunge kumi wa chadema.   Mshefa Pius     December 08, 2017     0   Comments Aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC, Jerry Murro amesema kutokana na uwezo wake katika mambo mbali mbali anaweza kujilinganisha na wabunge kumi  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Katika mahojiano na kipindi cha Maisha Mseto cha Times Fm, Jerry amesema kutokana na uwezo wake suala la ubunge kwake ni jambo rahisi tu sawa na kubofya button. “Mimi Jerry Murro mmoja ni sawa na wabunge 10 wa Chadema, nimewazidi kifikra, kinguvu, kipesa, maadili, kihoja na mambo mengine mengi sana” amesema Jerry Murro.  Katika hatua nyingine Jerry Murro amesema mwaka 2020 si ajabu kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Edward Lowassa wakirejea katika Chama cha Mapinduzi (CCM)

Ana Mghwira ajiunga CCM Zitto atoamachozi licha kubaki mwenyewe

MTEULE THE BEST Anna Mghwira Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, asubuhi hii ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) alipokaribishwa kuhutubia baada ya mkutano wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho (UWT) kufunguliwa rasmi na Rais John Magufuli mkoani Dodoma. Mghwira, mwanasiasa shupavu aliyekuwa mwanachama wa chama cha ACT-WAZALENDO amesema baada ya kufanyakazi kama Mkuu wa Mkoa chini ya serikali ya Rais Magufuli, ameweza kuiona CCM inayobadilika ambapo sasa inaonekana wazi kuwa chama hicho kinakataa rushwa na kinaweka maslahi ya Taifa mbele.  Mghwira alikuwa ni mwanamke pekee aliyegombea kiti cha ufrais kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, uliomwingiza madarakani Rais John Magufuli Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka kuwa  ndani ya chama chake (ACT) kuna watu wengi wakiwemo wanachama wa kutosha  akimaanisha hajabaki mwenyewe. Zitto amefunguka hayo akimjibu mfuasi wake wa kwenye mtan...

Ronaldo amshinda Messi atwaa tuzo ya Ballon D'or tena

Ronaldo atwaa tuzo ya Ballon D'or kwa mara ya tano Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa pili mfululizo usiku wa kuamkia leo. Ronaldo amemshinda mpinzani wake wa karibu Lionel Messi, katika tuzo hiyo na kuweza kuitwaa kwa mara ya tano na kuwa sawa na Messi ambae pia ametwaa kwa mara tano. Nyota wa Barcelona Lionel Messi, amepata nafasi ya pili huku mchezaji mahiri wa Psg ya nchi Ufaransa Neymar Jr,akiwa katika nafasi ya tatu Msimu uliopita Ronaldo aliisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya na ubingwa wa la Liga kwa mara ya kwanza toka toka mwaka 2012. Ballon d'Or ni tuzo ambayo imekua ikitolewa na jarida la nchini Ufaransa toka mwaka 1956 na kura hupigwa na waandishi wa habari wapatao 173, duniani kote Tazama video iliyompa ushindi huo Cristiano Ronaldo 2017 • 'The 5th Ballon D'or is mine' • Official Movie 2017_HD

Kiongozi mwingine akiapishwa litakuwa kosa la uhaini Kenya

MTEULE THE BEST Mwanasheria mkuu wa Kenya Prof Githu Muigai amesema jaribio lolote la kumuapisha kiongozi mwingine wa Kenya litakuwa ni uhaini wa hali ya juu. Prof Muigai amesema hayo huku kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga akisisitiza kwamba ataapishwa kuwa rais Jumanne wiki ijayo. Bw Odinga alitangaza mwezi uliopita kwamba ataapishwa na Mabunge ya Wananchi ambayo yalipendekezwa na muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa). Ingawa hakumtaja mtu yeyote, Prof Muigai, akiwahutubia wanahabari Nairobi, alisema shughuli hama hiyo ya kumuapisha kiongozi ambaye hajatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) haina msingi wowote kikatiba na kwamba itakuwa "bure na batili". "Sheria za jinai za Jamhuri ya Kenya zinazungumzia shughuli kama hiyo kuwa uhaini wa hali ya juu," amesema. "Wanaoshiriki watakuwa wanajihusisha katika uhaini wa hali ya juu, pamoja na wote wanaofanikisha shughuli kama hiyo." Adhabu ya kosa la uhaini kw...

Mchoro wa Yesu uliouzwa dola milioni 450 waelekea Abu Dhabi

Mchoro huo unaofahamika kama Salvator Mundi au (mkomboi wa dunia) - uliuzwa mjini New York kwa dola milioni 450. Mchoro wa miaka 500 wa Yesu ambao unaaminiwa kuwa wa Leonardo da Vinci, unapelekwa katika makavazi ya Louvre huko Abu Dhabi, Vyombo vya habari vinasema kuwa mchoro huo ulinunuliwa na mwanamfalme nchini Saudi Arabia. Mchoro huo unaofahamika kama Salvator Mundi au (mkomboi wa dunia) - uliuzwa mjini New York kwa dola milioni 450. Mnunuzi wake alishiriki kwenye mnada kwa njia ya simu katika mnada uliodumu kwa takriban dakika 20. Ndio mchoro uliouzwa pesa nyingi zaidi katika historia. Mnunuzi wake alishiriki kwenye mnada kwa njia ya simu katika mnada uliodumu kwa takriban dakika 20. Gazeti la The New York Times liliripoti kuwa ulinunuliwa na Bader bin Abdullah bin Mohammed bin Farhan al-Saud. Leonardo da Vinci alifariki mwaka 1519 na kuna chini ya michoro yake 20 iliyojulikana hidi sasa

Marekani yamuonya Odinga dhidi ya kujiapisha Kenya

Raila Odinga Marekani imemtaka kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga kuacha mpango wake wa kuapishwa kama rais wa nchi hiyo wiki ijayo. Odinga aliwasilisha kesi juu ya mapungufu katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti katika Mahakama ya Juu nchini humo ambayo ilibatilisha uchaguzi huo na kuagiza uchaguzi wa marudio ufanyike. Bw Odinga na muungano wake wa National Super Alliance hata hivyo walisusia uchaguzi huo wa 26 Oktoba ambapo Bw Kenyatta alitangazwa mshindi na mwishowe kuapishwa kwa muhula wa pili. Waziri msaidizi wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika, Donald Yamamoto ambaye alikuwa amezuru Kenya alimtahadharisha Bw Odinga na pia akahimiza kuwepo mashauriano kati yake na serikali iliyopo madarakani. Aidha alitahadharisha dhidi ya matendo ambayo yako nje ya katiba nchini humo. Baadhi ya viongozi wa serikali wameonya kuwa tukio hilo la kuapishwa linaweza kuhusishwa na uhaini. Mshauri wa Bw Odinga Salim Lone alipuuzilia mbali onyo hilo la Marekani na kusema ...

Majaliwa aizungumzia Dar es salaam itakavyobaki baada ya Serikali kuhamia Dodoma

MTEULE THE BEST Serikali imesema kwamba kuhamia Dodoma haiondoi hadhi ya Jiji la Dar es Salaam, na kwamba mji huo utabaki kuwa sehemu ya biashara. Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati akifungua ofisi ya Shirika la maendeleo ya Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa kuwepo kwa ofisi ya Umoja wa Mataifa mkoani Dodoma ni ishara ya kukamilika kwa serikali kuhamia rasmi mkoani humo. "Leo nafungua ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Dodoma, zaidi ya watumishi 2376 wameshahamia Dodoma, mimi tayari nimehamia mapema, Makamu wa Rais Samia Suluhu ataungana nasi mwishoni mwa mwezi huu , mwakani tunategemea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli atahamia huku", amesema Majaliwa. Pia ameongeza kwa kusema, "Umoja wa Mataifa una mchango mkubwa sana katika Taifa letu, imechangia mipango mingi ya maendeleo , mpango wa kwanza ulianza mwaka 2011, wakati huu wa pili umeanza 2016 na utaishia 202...

Marekani mbioni kukabiliana na tishio la Korea Kaskazini

MTEULE THE BEST Mshauri wa masuala ya usalama wa Ikulu ya White House nchini Marekani, HR McMaster, amesema kuwa Marekani iko mbioni kukabiliana na tishio kutoka Korea Kaskazini Uwezekano wa kutokea vita unaongezeka kila siku lakini vita sio suluhu pekee, aliuambia mkutano wa ulinzi. Matamshi yake yanakuja siku tatu bqada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la kwanza la kombora la masafa marefu katika miezi miwili kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Kombora hilo lilipaa mbali na makombora mengine ambayo yalijaribiwa awali kbala ya kuanguka katika bahari ya Japan. Kombora la Hwasong-15 lilipaa mbali zaidi na makomboa mengine ya awali HR McMaster ameitaka China kuiwekea vikwazo vya mafuta taifa hilo ili kufanya kuwa vigumu kwa Pyongyang kujaza mafuta makombora yanayofanyiwa majaribio. Korea Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kuchochea vita. Imetaja zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Korea kusini na Marekani kuwa la uchochezi na kwamba linaweza kusababisha vita. Uw...

Watu 13 waangamia kwenye ajali ya mashua Korea Kusini

MTEULE THE BEST Takriban watu 13 wamefariki baada ya mashua ya uvuvi kugonga na meli kubwa na kusababisha mashua hiyo kupinduka nje ya pwani ya Korea Kusini. Watu wengine wawili hawajulikani waliko na walinzi wa pwani ya Korea Kusini wanasema kuwa oporesheni ya kuwatafuta na kuwaokoa inaendelea. Mashua hiyo ya uvuvi ya Seonchang-1 ilikuwa imewabeba abiria 20 na wahudumia wawili wakati ajali hiyo ilitokea. Picha zilionyesha mashua hiyo ikiwa imepinduka. Ndege za helikopta na na meli kadhaa zinashiriki katika shughuli za kuitafuta. Kisa hicho kinatajwa kuwa kibaya ziadi nchini Korea Kusini tangu watu 15 waangamiae baharini eneo la Jeju mwaka 2015. Kabla ya mwaka huo feri ya abiria ilipinduka ambapo zaidi ya watu 300 walifariki wengi wao watoto wa shule.

Umoja kwa amri ya jumla ya Emirates na De Gea na Lingard

MTEULE THE BEST Jose Mourinho na kampuni walipeleka pigo kubwa kwa Gunners, matarajio, kasi na mstari kamili ambao hawakuwa nyumbani walionekana wakati mwingine kama wasioweza kushindwa. Licha ya adui au adui aliyekuja kucheza katika kile walichoona kama nyumba ya hofu katika rangi ya Holloway, kaskazini mwa London. Uwanja wa Emirates ulipungua mipaka kwa wachezaji wengi mpaka mechi ya leo, wakati mchezaji wa Manchester United akifika sehemu hizi za London Town, alikuja na tayari kutoa pigo kubwa kwa wakazi wa kuanzia kumi na moja. Ndiyo hii ni jitihada za kikundi lakini kwa ajili ya kutembelea United Boys wawili wa wachezaji wake kukamata alama zote katika mlinzi David De Gea na Jesse Lingard kuifunga kushinda muhimu na kuonekana kama tune up kwa wiki ijayo Manchester Derby. Hawa wawili wanapata heshima na kutoa katika kambiki wakati inahitajika, kama de de Gea akawa shujaa wa mechi baada ya kuacha pigo la shina 33 ambalo lilipatikana kutoka kwa washambuliaji wa Gun...