Mshukiwa aliyeabiri ndege kisiri inaaminika ameanguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways kutoka Nairobi kuelekea Heathrow, na kuanguka katika bustani moja huko kusini mwa London Lakini ni mara ngapi visa kama hivyo huhuhudiwa na hali huwa vipi wakati wa safari za aina hiyo? Ni mara ngapi visa hivi hutokea? Licha ya kwamba sio jambo la kawaida, hii sio mara ya kwanza kwa mtu kuingia katika sehemu za ndege wakati ndege hiyo ikisafiri na kujificha wakati wa safari ya kuelekea Uingereza. mwili ulipatikana katika bustani ilioko Offerton Road huko Clapham Kati ya Januari 2004 na Machi 2015, watu sita walioingia kwa siri katika ndegekatika uwanja wa ndege Uingereza walipatikana kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za shirika la viwanja vya ndege (CAA ). Mwingine mmoja alipatikana katika ndnai ya ndege ya Uingereza katika uwanja wa ndege ng'ambo. Takwimu kutoka shirika la viwanja vya ndege Marekani zimeashiria kuwa watu 96 wamewahi kujificha katika sehemu za ndege ...