Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya BURUNDI

Makala: Achana na Wasafi Festival; Diamond, Alikiba hadi Studio

Huwenda nyakati zikawalazimu Diamond Platnumz na Alikiba kuwa kitu kimoja kwenye muziki kwa sasa. Ni kipindi kirefu wameripotiwa kutoelewa ingawa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hilo.  Kwa sasa Diamond yupo katika pilika pilika za kuhakikisha tamasha lake la Wasafi Festival linafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wakati akieleza kuhusu ujio wa Wasafi Festival alieleza kuwa angetamani na Alikiba angekuwepo kitu ambacho kiliibua mjadala mpana zaidi.  Alikiba tayari amekubaliwa kuwa sehemu ya udhamini wa Wasafi Festival kupitia kinywaji chake cha Mo Faya. Wengi wamesema huu ni mwanzo nzuri kwa wasanii hawa kurudisha ushirikiano wao na kufanya vitu vikubwa zaidi.  Kwanini Studio    Hapo jana Diamond Platnumz akiwahojiwa na kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio nchini Kenya alisema si Alikiba kushiriki Wasafi Festival tu bali hata kufanya wimbo pamoja yupo tayari.  "sio tu Alikiba mtu yeyote ambaye anahisi kuna sehemu nikimuweka Diamond itanisaidia katika k...

Hatari tano kwa biashara Afrika Mashariki 2018

Kenya inarudi katika hali ya utulivu kisiasa baada ya uchaguzi wa rais uliochukua muda mrefu na uliokumbwa na misukosuko. Hata hivyo changamoto zitaendelea kuwepo mwaka huu kwa mashirika yanayohudumu nchini humo na Afrika Mashariki kwa ujumla. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la kitaalamu Control Risks linalochambua hatari na udhibiti wa hatari za kibiashara na uwekezaji. Daniel Heal ambaye ni mshirika mkuu wa shirika hilo katika kanda ya Afrika Mashariki, amesema "mwaka 2018 ni mwaka wenye matumaini kwa Kenya na Afrika Mashariki. Tayari tumeanza kuona imani ya wawekezaji ikirejea taratibu kufuatia udhibiti wa kisasa Kenya na azma katika miradi mipya ya miundo mbinu Kenya na katika kanda hiyo kwa jumla. Tunatarajia hili kuendelea hadi mwisho wa mwaka huu." Hata hivyo Daniel anasema nchini Kenya, hitaji la kulipa awamu ya kwanza ya mkopo wa fedha za Eurobond ambazo zilikuwa dola milioni 774.8, linapaswa kuishawishi serikali kudhibiti ukopaji na matumizi kabla deni kufi...

Nkurunziza ‘anataka kuongoza’ Burundi hadi 2034

MTEULE THE BEST Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amezindua kampeni ya kufanyika kwa kura ya maamuzi ambayo inatazamwa na jaribio la kutaka kusalia madarakani hadi 2034. Shirika la habari la AFP linasema mpango huo unahusisha kuidhinishwa kwa rasimu ya katiba ambayo itamuwezesha kuwania urais kwa mihula miwili zaidi ya miaka saba kila muhula. Muhula wa sasa wa Bw Nkurunziza unafikia kikomo 2020. Rais huyo aliwaambia wafuasi wake Jumanne katika kijiji cha Gitega kwamba wale wanaopinga juhudi zake "kwa maneno au kwa vitendo" watakuwa wameuvuka "mstari mwekundu". Kampeni hiyo imeanzishwa baada ya serikali kuzindua juhudi za kuchangisha fedha za maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Shirika la habari la AFP linasema mchango huo, ambao serikali inasema ni wa hiari, umeshutumiwa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu ambayo yamesema ni kama "wizi kwa mpango". Viongozi wa upinzani walio uhamishoni wanasema kura hiyo ya maoni itakuwa ka...