River Plate Bingwa wa Copa Libertadores , ilikuwa game ya kihistoria Bernabeu Fainali ya Kombe la Copa Libertadores kati ya River Plate na Boca Junior unaweza kuiita fainali ya kusisimua katika soka usiku wa December 9 2018, mvuto wa fainali hiyo unakuja kutokana na kuzikutanisha timu wapinzani ambao wamesabisha kiasi cha game hiyo kushindwa kuchezwa Argentina na kupelekwa katika jiji la Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mastaa kibao wa soka akiwemo Lionel Messi wa FC Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid , ulimalizika kwa River Plate kupata ushindi wa magoli 3-1, hiyo wanashinda taji hilo kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-3, kwani mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2. Ubingwa wa Copa Libertadores kwa River Plate unakuwa ni Ubingwa wao wa nne katika histori...