Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TPL

BAKULI LA YANGA LAENDELEA ILI WAWEZE KUPATA NAULI YA KUPANDA NDEGE

Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City Jumapili hii hivyo kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amewaomba wanachama kuichangia timu ili iweze kufafiri kwa ndege na kiasi kitakachopelea yeye ataongezea. Kikosi cha Yanga Zahera ambaye hayupo nchini amedai kitendo cha timu kusafiri tarehe 27 na kwenda kucheza tarehe 29 sio rahisi kwenda kwa basi hivyo ni lazima iende kwa ndege ili iweze kupata matokeo. ''Mimi kocha Mwinyi Zahera naomba wanachama waichangie klabu iweze kusafiri kwa ndege kwenda Mbeya ili tukacheze na tupate matokeo na mimi binafsi nitaongezea kiasi kitakachopelea'', amesema Zahera. Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera Aidha Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo amesema matokeo ya Yanga ni muhimu kwa wanachama na timu nzima ili kuendelea kuongoza ligi kwahiyo kila mmoja anayo sababu ya kuhakikisha timu inasafiri vyema. Yanga kwasasa inaongoza ligi ikiwa na alama 47 kwenye ...

TFF YA THIBITISHA TIMU HAZIJAPEWA PESA ZA UBIGWA

'Simba na Mtibwa hazijapewa fedha za ubingwa'' Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa katibu Mkuu wake, Kidao Wilfred, limeweka wazi kuwa mabingwa wa michuano ya kombe la shirikisho nchini, ambao ni Simba na Mtibwa Sugar bado hawajapewa fedha za ubingwa. Wachezaji wa Simba walipokabidhiwa ubingwa wa ligi kuu. Akionge leo na wana habari Kidao amefafanua mambo mbalimbali likiwemo hilo la fedha za zawadi ya mashindano hayo ambapo ameweka wazi kuwa hata Simba bado hawajapewa. ''Ni kweli Mtibwa Sugar hawajapata fedha zao milioni 50 za ushindi wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) msimu uliopita 2017/18 lakini hata Simba ambao ni mabingwa wa msimu wa 2016/17 nao hawajapata kuna vitu tunaweka sawa'', amesema. Kidao amesema kwamba sababu kubwa ni kuwa kuna vitu vya kimkataba baina yao na wadhamini vinafanyiwa marekebisho kutokana na uongozi kuwa mpya madarakani hivyo kuna mapitio ya kuboresha vipengele vya mkataba na fedha hiz...

Klabu bingwa Africa: Kinnah Phiri kuwinda Simba

Mbabane Swallows wamkabidhi Kinnah Phiri  mtihani wa Simba Kocha wa zamani wa Mbeya City, Kinnah Phiri amekabidhiwa jukumu la kuiongoza klabu ya Mbabane Swallows katika mechi dhidi ya Simba. Phiri amepewa jukumu hilo la muda mfupi kutokana na kocha mkuu wa Mbabane Swallows, Thabo Vilakati kutumikia adhabu ya kifungo cha mechi nne kutoka CAF kwa kosa la kumpiga muokota mpira. Simba itapambana na Mbabane Swallows katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumatano.

Simba: Lipuli FC Tunaikumbuka vizuri sana

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amesema kuwa timu yake imekiri kuwa bado wanakumbukumbu nzuri na namna ambavyo Lipuli ilivyokuwa klabu pekee iliyogoma kufungwa na Simba katika mechi zote mbili msimu uliopita.  Akiongea kuelekea mchezo wao wa ligi kuu kesho utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam, Manara ameweka wazi kuwa kocha wao Patrick Aussems anatambua uwezo wa Lipuli FC hivyo ameandaa kikosi kwaajili ya kusaka alama 3 na si vinginevyo.  ''Tunawajua Lipuli vizuri na tunafahamu ndio timu pekee iliyopata sare pacha msimu uliokwisha wa ligi lakini Simba ndio bingwa wa taifa hili na tunaingia kesho tukiwa kamili hivyo mashabiki wa Simba waje Taifa kesho saa kumi waone mpira wa raha kutoka kwa kocha wetu Aussems'', amesema.  Kwa upande wa Lipuli Fc kupitia kwa msemaji wao Festo Sanga wamesema wamejiandaa vyema kwaajili ya kushindana kutafuta alama 3 dhidi ya wenyeji wao Simba.  Msimu uliopita Lipuli haikufungwa na Simba baada ya kutoka sare ya...

TPL: USHINDI WA YANGA LEO WAPELEKA MSIBA MZITO SIMBA

Yanga yaishusha Simba Kikosi cha timu ya Yanga kimeweza kuishusha timu Simba na kufikisha pointi 29 baada ya kuwafunga Mwadui FC mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage.  Na kwamatokeo hayo Yanga wamefanikiwa kuendeleza rekodi yao kwa kucheza michezo 11 bila kupoteza.  Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji Herieter Makambo na Mrisho Ngasa akifunga bao la pili la ushindi.  Yanga wamecheza leo bila ya kuwa na wachezaji wao kama Ibrahim Ajibu, Kelvin Yondani, Beno Kakolanya na Papy Tshishimbi