Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto nchini Tanzania imekiri kuwepo kwa magonjwa wa homa ya Chikungunya na Dengue katika taifa hilo kubwa kabisa Afrika Mashariki. Akitoa taarifa kwa wadau na waandishi wa habari mapema leo (Juni 25), Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amebainisha kuwa mnamo tarehe 20 Juni wasafiri wanne wa familia moja waliotokea Mombasa, Kenya, walibainika kuwa na ugonjwa huo kwenye kituo cha mpakani cha Holili, mkoani Kiliamanjaro. Awali jumla watu sita walibainika mwezi wa Januari mkoani Tanga kuwa na ugonjwa wa Chikungunya kupitia kwenye kituo cha mpakani cha Horohoro wakitokea pia Mombasa. Wakati huo huo, Tanzania imethibitisha pia kuwepo kwa homa ya Dengue, ambapo hadi sasa watu 226 wamethibitika kuwa na ugonjwa huo katika mkoa wa Dar es Salaam pekee, ambao ni kitovu cha kiuchumi na biashara. Kwa mara ya kwanza homa ya Dengue iliripotiwa nchini humo mwaka 2010