Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CLOUDS

Wamiliki wa WASAFI TV wajulikana, hisa za Diamond ni asilimia 45

Kituo hicho kipya cha televisheni kimezua mjadala kuhusu wamiliki wake tangu kilipoanza matangazo ya majaribio, baadhi wakisema kinamilikiwa kwa asilimia 100 na nyota huyo wa Bongo Fleva. Dar es Salaam. Ni Diamond Platnamuz au Joseph Kusaga? Ndio mjadala mkubwa uliodumu tangu mwanamuziki huyo nyota wa miondoko ya Bongo Fleva aanze kukitangaza kituo kipya cha televisheni cha Wasafi TV. Baadhi wanadai mmiliki ni Diamond na wengine wanasema Kusaga, mmoja wa manguli katika biashara ya burudani na ofisa mtendaji mkuu wa Clouds Media, wakidai anamtumia nyota huyo wa Bongo Fleva kutangaza televisheni hiyo mpya. Wakati mjadala huo ukiendelea, Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano (TCRA) imetoa tangazo linalodokeza majibu ya mjadala huo. Katika tangazo lake kwa umma kutaka maoni au pingamizi kuhusu maombi ya leseni ya Wasafi TV, mamlaka hiyo imewataja wamiliki watatu wa televisheni hiyo, ambayo tayari ipo hewani. TCRA imemtaja mtu anayeitwa Juhayna Zaghalulu Ajmy na ambaye ni Mtanzania, ...