Askofu Mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa.

KILINGENI Vatican NEWS Askofu Mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa. Ask.Caccia:Hakikisha mazingatio ya maadili ya AI yawe msingi na usambazaji wa maendeleo Vatican inasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba maendeleo na matumizi ya AI daima yanabaki katika huduma ya wanaume na wanawake,kukuza udugu na kuhifadhi fikra makini na uwezo wa utambuzi.Haya yameo katika hotuba ya Askofu Mkuu Caccia,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa huko New York,Marekani aliyotoa kwenye kikao maalum cha ECOSOC kuhusu Akili Mnemba jijini New York -Marekani tarehe 6 Mei 2025. Na Angela Rwezaula -Vatican. Askofu Mkuu Gabriele Caccia Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa alitoa hotuba yake katika Mkutano Maalum wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) ambalo ni jukwaa kuu la Umoja wa Mataifa, kuhusu Akili Mnemba tarehe 6 Mei 2025 huko mjini New York, Marekani. Katika Hotuba ya kikao cha kwanza kilichoongozwa na mada ya “Mitindo inayo...