Wafadhili wanakutana mjini Geneva Uswisi Ijumaa katika harakati za kuchangisha dola bilioni 1.7 kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo inakabiliwa na mzozo. Wataalam wanasema huenda mzozo huo ukapindukia na kuwa janga kubwa. Mkutano huo unakuja wakati kukiwa na hofu kwamba mizozo ya kikabila, ufisadi na hali mbaya ya usalama ni mambo yanayozusha hofu ya umwagikaji damu. Kwa wale walioachwa bila makao, kitisho ni cha kweli. Raia mmoja wa Congo alielezea mzozo wa kikabila katika mkoa wa Ituri kwa kusema, "ni kama wakati tulipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe." Kulingana na makadirio ya shirika la msalaba mwekundu karibu Wacongo 70,000 wamekimbilia Uganda kwa kuuvuka mto Albert tangu Januari. Ituri ni mkoa mmoja tu kati ya mingi ambayo makundi yaliyojihami na wahalifu wanawasumbua raia. Ukosefu wa usalama umezidisha idadi ya wakimbizi wa ndani ya nchi Zaidi ya hayo kuna mzozo wa kisiasa unaozunguka suala la urais ambapo watu wengi wanamtaka rais Joseph...