Huwenda nyakati zikawalazimu Diamond Platnumz na Alikiba kuwa kitu kimoja kwenye muziki kwa sasa. Ni kipindi kirefu wameripotiwa kutoelewa ingawa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hilo. Kwa sasa Diamond yupo katika pilika pilika za kuhakikisha tamasha lake la Wasafi Festival linafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Wakati akieleza kuhusu ujio wa Wasafi Festival alieleza kuwa angetamani na Alikiba angekuwepo kitu ambacho kiliibua mjadala mpana zaidi. Alikiba tayari amekubaliwa kuwa sehemu ya udhamini wa Wasafi Festival kupitia kinywaji chake cha Mo Faya. Wengi wamesema huu ni mwanzo nzuri kwa wasanii hawa kurudisha ushirikiano wao na kufanya vitu vikubwa zaidi. Kwanini Studio Hapo jana Diamond Platnumz akiwahojiwa na kipindi cha Mambo Mseto cha Citizen Radio nchini Kenya alisema si Alikiba kushiriki Wasafi Festival tu bali hata kufanya wimbo pamoja yupo tayari. "sio tu Alikiba mtu yeyote ambaye anahisi kuna sehemu nikimuweka Diamond itanisaidia katika k...