Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MATIBABU

MAPACHA WATANZANIA WALIOUNGANA WATENGANISHWA

  MAPACHA wa Tanzania walioungana, Anishia na Melanese, wametenganishwa nchini Saudi Arabia Desemba 23, 2018, na hali zao zinaendelea vizuri kwa wakati huu.   Jumanne Desemba 25, 2018 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Aminiel Aligaesha amethibitisha mapacha hao kutenganishwa.   Kwa mujibu wa gazeti la nchini Saudi Arabia, saudigazette.com mapacha hao walitenganishwa na jopo la wataalamu 32 kwa muda wa saa 13.   Upasuaji huo uliofanyika katika hospitali ya Mfalme Abdullah, (King Abdullah Children’s Specialist Hospital) iliyopo katika mji wa Riyadh (King Abdulaziz Medical City), uliongozwa na Dk Abdullah Al-Rabeeah.   Mapacha hao wa kike waliozaliwa katika Kituo cha Afya cha Missenyi, Kagera, Januari 2018,  walipofikishwa Saudi Arabia walifanyiwa vipimo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya kuona uwezekano wa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha

Rais wa Tanzania afiwa na dada yake

Rais Magufuli alipoenda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Dada yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza. Hapo jana Rais Magufuli alienda kumtembelea dada yake akiwa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) katika hospital hiyo ya Bugando na rais alisema kwamba hali ya dada yake sio nzuri. Bi.Monica Magufuli alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63 (alizaliwa tarehe 25 Novemba, 1955) na ameacha watoto 9 na wajukuu 25

Msichana apambana na malaria kwa mishumaa

Yumkini sasa ugonjwa hatari wa malaria unaweza ukawa historia nchini Tanzania, kutokana na mbinu mbalimbali zinazoibuliwa na wananchi wa kawaida kukabiliana na ugonjwa huu sugu katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Serikali imekuwa ikifanya juhudi katika kukabiliana na malaria kwa kunyunyizia dawa za kuuwa viluwiluwi vinavyosababisha ugonjwa huo kwenye makaazi ya watu, kugawa vyandarua vyenye dawa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujikinga na ugonjwa huu.  Licha ya jitihada hizi kusaidia, lakini tatizo la msingi bado liliendelea kuwapo. Nalo ni uwelewa mdogo wa walengwa kwenye kampeni yenyewe. Lakini sasa matumaini ya kutokomeza malaria yamezaliwa upya baada ya kutengenezwa kwa mishumaa inayofukuza mbu, hatua itakayoongeza nguvu katika juhudi za kupambana na ugonjwa huu. Beatrice Mkama ni mjasiriamali mwenye ndoto za kuisaidia jamii yake katika kuitokomeza malaria iliyosababisha kuondokewa na ndugu zake waliofariki baada ya kuugua ugonjwa huo. Beatrice, ambaye kitaaluma...

"Wabunge hawafuati utaratibu"- Pius Msekwa

Sakata la matibabu ya Wabunge, Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa Wabunge hawafuati utaratibu kwa kufanya maamuzi yao binafsi. Msekwa amefunguka hayo wakati akizungumza na eatv.tv na kusema kuwa kuna taratibu za matibabu kwa Wabunge na hairuhusiwi kutibiwa hospitali yoyote kwa uamuzi binafsi lakini wanashindwa kufuata miongozo hiyo na kuibua migogoro. “Mbunge akiugua huwa anapelekwa hospitali ya serikali na endapo akitakiwa kuhamishwa hospitali atapewa rufaa na lazima bunge liwe na taarifa hakuna anayefanya maamuzi yake binafsi alafu anahitaji kulipwa”,  amesema Msekwa. Aidha, Msekwa ameongeza kuwa hakuna upendeleo kama ambavyo Kambi ya Upinzani Bungeni inavyodai na imekuwa hivyo tangu mwanzo kwa kuwa fedha zinazotumika ni za umma na zinataratibu zake. Hayo yamejiri baadaya kuwepo kwa madai kuwa Wabunge wa upinzani hawapewi kipaumbele pindi wanapotakiwa kupatiwa matibabu.